Tunamaliza na tunaanza mwaka 2021 bila Mzee Mkapa

27Dec 2020
Nkwazi Mhango
Nipashe Jumapili
FIKRA MBADALA
Tunamaliza na tunaanza mwaka 2021 bila Mzee Mkapa

KWANZA, kwa kipekee zaidi, tutume safari na heri za Noeli na Mwaka Mpya 2021 kwa wapenzi wote wa safu hii pia tuwaalike katika kumkumbuka mzee wetu Benjamin William Mkapa, Rais wa Awamu ya Tatu aliyetutoka tarehe 24 Julai, 2020.

Kifo cha mzee Mkapa kilitokea wakati safu hii haijarejea hewani. Tunaomba kufunga mwaka huu kwa; mosi, kutoa salamu za rambirambi kwa taifa na familia. Pili, kama kumbukizi la mzee Mkapa, safu hii leo imeamua kudurusu namna atakavyokoswa hasa mwaka 2021 tunaotegemea kuanza siku chache zijazo inshallah.

Kwa tuliomfahamu mzee Mkapa kama gwiji la diplomasia na usuluhishi, kifo chake si pigo kwetu tu bali kwa nyanja ya diplomasia na usuluhishi Afrika na duniani kote. Binafsi, mzee Mkapa alinisaidia mawazo wakati naanza kusomea shahada yangu ya uzamivu (PhD) kwenye masuala ya amani na migogoro pale nilipomwomba anipe uzoefu wake...kwa habari zaidi soma kupitia https://epaper.ippmedia.com