Tuwe na magulio salama au hatarishi?

27Dec 2020
Joseph Kulangwa
Nipashe Jumapili
MADONGO YA MGAGAGIGIKOKO
Tuwe na magulio salama au hatarishi?

KAMA kuna jambo linamnyima usingizi Rais John Magufuli, ni hili la wanyonge kunyimwa haki. La wanyonge kunyimwa fursa zilizopo, za kujikwamua kiuchumi.

Tangu aingie madarakani mwaka 2015, Rais Magufuli alisisitiza watu wa hali ya chini kutonyanyaswa, akishinikiza wafanyabiashara ndogo mijini-wamachinga, kuachwa wafanye shughuli zao bila dhahama.

Kama hiyo haitoshi, hatimaye akaona kama anachokisema pengine hakieleweki, akaamua kuwatengenezea vitambulisho maalumu, ambavyo hivi sasa vinaboreshwa ili wavitumie kwa fursa zaidi.

Alitoa pia maelekezo ya kuondolewa kwa tozo mbalimbali walizokuwa wakitozwa wakulima vijijini, hasa walipokuwa wakisafirisha mazao yao ya chakula, huku akisisitiza kwa kauli ya “wakati analima hukumsaidia, iweje anavuna unamfuata kumkandamiza kwa kodi!”...kwa habari zaidi fuatilia kupitia https://epaper.ippmedia.com