Ujasiriamali chakula muhimu, lakini usafi mazingira lazima

31Jul 2020
Yasmine Protace
Nipashe
Muungwana Lazima Nilonge
Ujasiriamali chakula muhimu, lakini usafi mazingira lazima

AFYA ni kitu muhimu katika mwili wa mwanadamu. Ndilo linamhakikishia binadamu afya bora na amani.

Hapo ndipo kunazaliwa haja ya wajasiriamali chakula ambao ni wengi katika maeneo ya mijini na kokote kwenye shughuli za kijamii na kipato, mathalan stendi ya basi, panakotakiwa kuhakikishwa biashara inaandaliwa katika mazingira bora na salama.

Vitu vya usafi wa biashara vinaangaliwa sana na wataalamu wa masuala ya afya na lishe. Hiyo inatokana na kujali afya za walaji na inapobainika kuna uchafu katika maeneo hayo wahusika wanapaswa kuchukuliwa hatua kama faini.

Ili mhusika asitozwe faini, sehemu ya vigezo vya kisheria anatakiwa azingatie suala la usafi katika maeneo yake ya biashara.
Si ajabu kukaguliwa maeneo mbalimbali, mtu atakuta baadhi hawazingatii kabisa suala la usafi.

Kutozingatia suala la usafi kunasababisha walaji wanaoendelea kula chakula na kuuzwa matunda ambayo yamekuwa yakilambwa. Si jambo jema.

Uhakikishaji afya za walaji zinakuwa salaam. Inatakiwa kuzingatia kanuni za usafi na inazingatia pande zote mbili, yaani mlaji na muuzaji.

Tunaposema mlaji tuna maana mlaji asile bidhaa yoyote inayofanyika katika mazingira machafu. Muuzaji naye hatakiwi kufanya biashara katika maeneo yasiyofaa.

Katika mifumo yetu kijamii kumekuwapo mafunzo yanayotolewa kwa makundi hayo, ili kuhakikisha wanaandaa vyakula katika maeneo safi na salama, lengo likiwa ni kuwapatia walaji chakula kilicho salama na kisafi.

Inapokuwapo ongezeko la biashara za bidhaa kama vyakula, matunda na kushuhudia wachoma nyama na mishikaki, baadhi ya wafanyabiashara wamekuwa wakifanya biashara katika maeneo yasiyofaa.

Ni maeneo yanayokutwa na hitilafu kama mifereji ya majitaka na unakuta wafanyabiashara wa mishikaki, matunda na wauza samaki mbichi na za kukaanga wanaendelea kana kwamba hakuna kitu.

Tunapokuwa tunafanya biashara kuna mambo yasiyo sahihi. Kuna maeneo yanashangaza, bidhaa kama matunda yamepangwa katika meza.

Unaweza kushangaa chini ya eneo kuna mtaro wa maji machafu na yanayotoa harufu mbaya, isiyoendana na usafi ya mazingira.

Biashara inapofanyika upande wa pili wa shilingi, walaji nao wajali afya zao inakuwa hatarini. Biashara inafanyika katika mazingira yasiyofaa, hivyo kujali maslahi ya walaji.

Kwa kufanya hivyo wanaweza kuwasababishia walaji kupata ugonjwa wa tumbo kutokana na ulaji vitu vilivyoandaliwa katika mazingira yasiyofaa.

Niseme biashara ya mlo na usafi wa mazingira, ni jambo linaloendana kwa ubia. Ifanyiwe kazi.