Vipimo vyenye ubora vitawalinda walaji

26May 2016
Jackson Kalindimya
Nipashe
Mjadala
Vipimo vyenye ubora vitawalinda walaji

UZALISHAJI wa bidhaa mbalimbali unaendelea nchini Tanzania na duniani kwa ujumla.

Katika zama hizi za ushindani wa soko huria kila siku na mara kwa mara, bidhaa zinaingizwa nchini kwa lengo la kushindana na bidhaa nyingine kwa kuzingatia kuwa, dunia sasa ni kama kijiji kikubwa kinachoshirikiana maarifa na taarifa.

Mazingira hayo, yanasababisha upatikanaji wa bidhaa nyingi sokoni zikiwemo halali na haramu na kuwaathiri walaji hasa wale wasio makini.Mazingira hayo ndiyo yanalazimisha kuhakikisha umuhimu wa kuwepo maabara maalum ya kupima vipimo

Hivi karibuni yalifanyika maadhimisho ya Siku ya Ugezi (Metrology) duniani katika nchi mbalimbali Tanzania ikiwa mojawapo.Kauli mbiu ya maadhimisho hayo ni ‘Vipimo katika Dunia ya Mabadiliko “

Kimsingi lengo la kauli mbili hiyo ni kuwafumbua wa macho na kuwakumbusha umuhimu wa kuzingatia vipimo kwa ajili ya kuleta mabadiliko hasa katika bidhaa na huduma.

Kaimu Mkuu wa wa Kitengo cha Maabara ya Vigezi (Metrology Laboratory) Vida Rusimbi katika madhimisho hayo alisema kuwa mkataba huo wa kimataifa ulitiwa saini na mataifa mbalimbali huko Ufaransa, May 20,1875 na baadaye kuridhiwa na Tanzania.

Tangu mkataba huo uliporidhiwa nchi mbalimbali zilikubaliana kuhusu vipimo na kusaini mkataba unaoelekeza matumizi ya vipimo vya aina moja, lengo ni kuondoa mkanganyiko wa matokeo ya vipimo tofauti ambao umekuwa ukiziathiri nchi nyingi.

Mkataba huo unazitaka nchi husika kuzingatia utekelezaji wake (SI units) ambao kwa Tanzania dhamana hiyo ipo chini ya Shirika la Viwango Tanzania (TBS) likiwa na maabara maalum ya kuhakikisha kuwa inapima na kukagua vipimo vyote ili kuhakikisha kuwa vinazingatia sheria.

Matuko ya watu kuuziwa bidhaa zisizozingatia ubora una madhata makubwa kwa watumiaji na hata kuchangia umaskini wao.Tuna viwanda vingi vikubwa na vidogo nchini ambavyo vinazalisha bidhaa muhimu kwa ajili ya matumizi ya walaji pamoja na bidhaa.

Kama bidhaa hizo zitaachwa kuendrelea kuzalishawa kiholoela ni kwamba madhara yake ni makubwa na mabaya sana.Ndio maana nchi mbalimbali baada ya kupima na kuona hatari inayowakabili watumiaji na nchi kwa ujumla ikaamua kuja na mkakati wa pamoja kuhakikisha kuwa kuna kuwa na maabara maalum ya kupima vipimo hivyo na kuhakikisha kuwa vinakuwa na ubora unaotakiwa ili kuwalinda walaji.

Uanzishwaji wa maabara ya Ugezi katika Shirika la Viwango Tanzania(TBS) dhamira yake ni kuhakikisha kuwa inadhibiti na kutunza viwango vya vipimo vya kitaifa na kimataifa hivyo kuifanya nchi yetu kupiga hatua muhimu ya kuhakikisha kuwa bidhaa zote zinazoingizwa nchini zinakaguliwa ili kuhakikisha kuwa zinazingatia vipimo bora klwa mujibu wa makubaliano ya kimataifa.

Maabara hiyo inahakiki usahihi wa vipimo vya bidhaa zao wakati wote kwa ajili ya biashara,mizani na bidhaa nyingine hivyo kuwafanya watu wanunue bidha ahalisi kulingana na thamani ya fedha zao.

Hii ni kuhakikisha kuwa mzalishaji anapozalisha bidhaa kama vile mabati,saruji au aina nyinginezo azalishe kwa kuzingatia vipimo vinavyotakiwa ili kuepusha madhara ambayo yamekuwa yakijitokeza kwa bidhaa ambazo zimekuwa zikizalishwa bila ya kuzingatia vipimo na kuathiri maisha nauchumi kwa ujumla.

Kimsingi maabara hiyo inelenga kumlinda mlaji au mtumiaji wa bidhaa pamoja na mazingira yake hasa kwa kuzingatia usahihi wa vipimo.

Ndio maana , Mkurugenzi Mkuu wa TBS, Joseph Masikitiko anasema kuwa kuwa maabara hiyo inazingatia vipimo vya kitaifa na kimataifa ili kuhakikisha kuwa suala zima la usahihi na vipimo mbalimbali linazingatia na kila mdau wa vipimo na mtumiji wa bidhaa zinazohitaji vipimo.

Pamoja na kuwepo kwa maabara hiyo nchini hakutakuwa na maana kama wadau na wananchi kwa ujumla hawatatoa ushirikiano wa kufichua wazalishaji na watu wote wanaozalisha au kuingiza bidhaa nchini ambazo hazizingatii ubora wa vipimo .

Kila mtu katika nafasi yake anatakiwa kutoa ushirikiano wa kuwaumbua watu wote ambao hawatumii vipimo halali vyenye ubora katika kuzalisha mali hata kusababisha athari mbaya kwa watumiaji huku wakijikusanyia utajiri haramu siku hadi siku.

Tanzania bila ya vipimo visivyo na ubora inawezekana kama tu kila mtu atatoa ushirikiano wa kuwafichua watu wote wanaokwenda kinyume cha sheria na mikataba ya kitaifa na kimataifa.Linalowezekana leo lisingoje kesho, timiza wajibu wako.