Watanzania tukumbatiane maisha yaendelee

01Nov 2020
Joseph Kulangwa
Nipashe Jumapili
FIKRA MBADALA
Watanzania tukumbatiane maisha yaendelee

MICHEZO miwili ninayoipenda sana maishani mwangu ni soka na masumbwi. Usiniulize kwa nini, kwa sababu ukiniuliza sitakupa jibu nyoofu. Nitakwambia naipenda tu kwa sababu naipenda.

Lakini kwa kifupi inanifurahisha, kwa sababu ni michezo ya ushindani inayohusisha timu mbili au watu wawili wanaochuana, chini ya mwamuzi au waamuzi.

Kwa kweli kuangalia soka na kuangalia masumbwi kunavutia na kuhamasisha. Kunaburudisha na kustarehesha, hasa pale mashabiki nao wanapokuwa wamejigawa sehemu mbili, kila upande ukishangilia uupendao.

Hutokea mara zingine mashabiki kucharuka na kukabana mashati na hata kutoana ngeu na damu. Kisa ni mihemko ya michezo yenyewe, hasa pale michuano inapokuwa imekamata na mshindi hatabiriki.

Kazi huwa pevu kwa waamuzi kuamua nani ni nani, hapo ndipo pia mashabiki hucharuka na kutaka kuingia akilini mwa waamuzi, ili kuamua wanachokitaka wao. Mshikemshike hutawala viwanjani na ulingoni.........kwa habari zaidi tufuatilie kupitia epaper.ippmedia.com