Samatta aliondoka nchini juzi akisindikizwa na Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Selestine Mwesigwa.
Hii ni mara ya kwanza kwa Tanzania kutoa mwanasoka kuingia hatua ya mwisho kuwania tuzo hizo zinazoandaliwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF).
Nyota huyo wa zamani wa Simba, atashindana na mchezaji mwenzake TP Mazembe katika nafasi ya kipa, Robert Kidiaba wa DRC na Bounedjah Baghdad raia wa Algeria
anayecheza soka na Klabu ya Etoile du Sahel ya Tunisia.
Meneja wa mchezaji huyo, Jamal Kasongo alisema juzi kabla Samatta kuondoka kuwa ameshindwa kuongozana na mchezaji huyo, badala yake Mwesigwa ndiye atakayempa sapoti