Shilole: Mmh Mziwanda wa nini?

13Jan 2016
Lete Raha
Shilole: Mmh Mziwanda wa nini?

JEURI! Nyota wa muziki wa kizazi kipya, Zuwena Mohamed a.k.a Shilole, amesema kuwa hawezi kurudi nyuma baada ya kuachana mpenzi wake wa zamani, Nuh Mziwanda, na badala yake anasonga mbele.

SHILOLE

Amesema kuwa mwaka huu ameamua kubadilika na kufanya mambo kiutu uzima na ndiyo maana akaachana na Mziwanda na kupata mchumba mwingine msanii, Eddy Kenzo wa Uganda, ambaye huenda wakafunga naye ndoa miezi ya usoni.
Shilole amesema hayo akidai baadhi ya watu wamekuwa wakimtaka arudishe moyo nyuma ili ikiwezekana arudiane na Mziwanda ambaye wamedumu naye kwa muda mrefu.
"Nimeshaamua na siwezi kurudi nyuma kwani tayari nimeshapata mchumba mpya ambaye siyo siri alikuwa akinipenda siku nyingi, lakini bahati mbaya nikawa ninampotezea hadi akanitungia wimbo," alisema Shilole.

Habari Kubwa