Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akisalimiana na watoto baada ya kushiriki Ibada ya Eid El Fitr kwenye Msikiti wa Anwar, Msasani jijini Dar es Salaam jana. PICHA: OWM Sehemu ya waumini wa dini ya Kiislamu Mkoa wa Dodoma, wakishiriki swala ya Eid El Fitr, katika Uwanja wa Jamhuri jijini humo jana. PICHA: IBRAHIM JOSEPH Sehemu ya kinamama wakishiriki swala ya Eid El Fitr katika viwanja vya Jamhuri jijini Dodoma jana. PICHA: IBRAHIM JOSEPH Baadhi ya waumini wa dini ya Kiislamu wilayani Muheza, Mkoa wa Tanga, wakichagua vazi kanzu baada ya kutoka katika swala ya Eid El Fitr katika Msikiti Mkuu wa Ijumaa, wilayani humo jana. PICHA: STEVEN WILLIAM Mkazi wa Mtaa wa Alhabasi wilayani Muheza mkoani Tanga, maarufu Mama Habiba (kulia), akiandaa mahanjumati katika soko kuu Muheza Juu katika kusherehekea sikukuu ya Eid El Fitr jana. PICHA: STEVEN WILLIAM Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, akipokea heshima za Baraza la Eid El Fitr kwa gwaride Maalum la Jeshi la Polisi Kikosi cha FFU, katika viwanja vya Ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdulwakil Kikwajuni Zanzibar jana. PICHA: IKULU ZANZIBAR