Tambwe: Ngoma anatisha

23Jan 2016
Faustine Feliciane
Nipashe
Tambwe: Ngoma anatisha

Amissi Tambwe anaongoza safu ya wafumani nyavu hatari wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu, lakini mshambuliaji huyo wa Yanga anajona si lolote mbele ya Donald Ngoma.

Tambwe, mchezajin wa zamani wa Simba na Vital'O, alisema jana Ngoma aliyejiunga na Yanga msimu huu akitokea Zimbabwe, ndiye mchezaji anayemkubali kwa sasa kwenye ligi hiyo.

Mrundi huyo alipiga ‘hat- trick’ yake ya pili msimu huu, Yanga iliposhinda magoli 5-0 dhidi ya Majimaji na kumfanya afikishe mabao 13 baada ya mechi 15.

"Hata hivyo, mkali huyo wa vichwa, alisema: "Ngoma ni zaidi ya mshambuliaji kwenye timu yetu, ana kila kitu, pia ni msaada kwa washambuliaji wengine, kwa kweli kwangu ndiye mchezaji bora kwenye ligi kwa sasa," alisema Tambwe.

Alisema magoli yake mengi yanachangiwa kwa kiasi kikubwa na nyota huyo wa zamani wa FC Platinum ya Ligi Kuu ya Zimbabwe.

"Tunapoingia kwenye eneo la hatari la timu pinzani anajua nini cha kufanya, alazimishi kufunga, anachojali ni kuona timu inapata ushindi, Ngoma ni mtu mzuri sana," alisema zaidi Tambwe.

Habari Kubwa