Uchaguzi meya Dar umetoa somo kwa wanasiasa

20Jan 2016
Sabato Kasika
Nipashe
Uchaguzi meya Dar umetoa somo kwa wanasiasa

BAADA ya kuahirishwa mara kadhaa, hatimaye uchaguzi wa meya na naibu meya katika manispaa za Kinondoni na Ilala, jijini Dar es Salaam umefanyika kwa utulivu na amani.

madiwani wa dar es salaam

Uchaguzi huo ulifanyika Jumamosi iliyopita kwa kufuata taratibu ambazo imekuwa zikitumika siku zote za kuwashirikisha wapigakura kata na majimbo husika husika bila kuhusisha wengine kutoka nje ya maeneo hayo kama ambavyo ilitaka kutokea
Manispaa hizo kwa sasa ziko chini ya upinzani baada ya wagombea wa nafasi hizo kutoka vyama hivyo kuibuka na ushindi kutokana na wingi wao ambao umetokana na Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba mwaka jana,.
Kwa mazingira yalivyokuwa, kulikuwa na kila dalili za upinzani kushinda katika uchaguzi huo kutokana na kuwa na madiwani wengi ingawa kulikuwa na figisufigisu ambazo ziliashiria kuuvuruga.
Lakini mwishowe kilichotokea ndicho hicho kwamba upinzani umeibuka na ushindi katika uchaguzi huo ambao kama nilivyosema ilijawa na vituko vya kila aina vikiwamo vya kuleta wapigakura kutoka Zanzibar ili kuja kuongeza nguvu.
Kwa matokeo ya uchaguzi ninaweza kusema kuwa wanasiasa wanapaswa kujifunza kwamba asiyekubali kushindwa sio mshindani, kwani kwa hali ilivyokuwa kulikuwa kuna kila dalili kwamba upinzani ungeshinda kutokana na wingi wao.
Lakini cha kushangaza ni kwamba walitokea baadhi yua wanasiasa na kuanza kuandaa mbinu za kutaka kulazimisha ushindi huku wakijua wazi kuwa ni wachache.
Hii ilionyesha kuwa hawakuwa tayari kushindwa ingawa ni wachache, lakini mwisho wake wamejikuta wakiangushwa vibaya katika uchaguzi huo ambao ulikuwa na mvuto wa aina yake kuafuatia kuahirishwa mara kadhaa.
Ni kweli kwamba chama kinaweza kuwa na wapigakura wengi lakini siku ya uchaguzi kikashindwa, lakini hiyo katika asilimia ninaweza kusema kuwa ndogo sana na sio ya kutegemea.
Hivyo ndivyo CCM walikuwa wanataka kutumia kwamba pamoja na wingi wao, upinzani hawakutakiwa kujihakikishia asilimia kubwa ya ushindi kwa vile anaweza kuweka mgombe ambaye hakubaliki akajikuta anabwagwa.
Kama nilivyosema, hiyo ni asilimia ndogo sana labda ile iliyokuwa ikilalamikiwa na kuleta wapigakura kutoka nje ili kuongeza nguvu, lakini vinginevyo sio rahisi kwa watu ambao wanafanya kila kukiondoa chama tawala halafu wageuke kukiunga mkono!
Uchaguzi umemalizika na sasa kilichobaki ni madiwani meya na manaibu wao kufanya kazi walizotumwqa na wananchi na pia wa uchaguzi huo uwe chachu kwa wanasiasa kuheshimu demokrasia.
Ninatambia kwamba kura ni siri ya mtu ana haki ya kuchagua kiongozi anayemtaka, lakini kitendo cha kutaka kuleta wapigakura kutoka nje ya maeneo husika kilikuwa ni sawa na kutoheshimui demokrasia.
Kilichotakiwa kufanywa ni kushawishi kwa njia halali wapigakura wawachague kuliko kusaka watu wasionhusika ili nao wapige kura kwa lengo la kusaka ushindi ambao kimsingi sio halali.
Kama vile ambavyo wananchi waliwaamini na kuwachagua, basi madiwani nao walitakiwa vizuri imani hiyo kuwaletea meya na manaibu meya kwa uhuru na haki bila kuongeza nguvu kutoka nje.
Kufanya hivyo ni sawa kulazimisha ushindi pasipo na dalili za kushinda na pia asiyekubali kushindwa sio mshindani, hivyo uchaguzi wa meya chachu ya kuheshimu demokrasia.
Siyo CCM wala upinzani, vyama vya siasa havitakiwi kulazimisha ushindi wakati vikijua wazo kuwa kuna kila dalili za kushindwa, kufanya hivyo ni sawa na kutoheshimu maamuzi ya wapigakura.