Walcoth miaka 10 magoli 53 Arsenal

20Jan 2016
Nipashe
Walcoth miaka 10 magoli 53 Arsenal

Theo Walcott anatimiza mulongo akiwa mchezaji wa Arsenal tangu winga huyo wa timu ya Taifa ya England ajiunge na Gunners akitokea Southampton tarehe kama ya leo mwaka 2006.

Theo Walcott

Baada ya kutua kwenye klabu hiyo akiwa na umri mdogo na asiye na uzoefu wa kucheza michuano mikubwa, Walcott amejengwa na kuwa mmoja wa mawinga hatari barani Ulaya na sasa ni mchezaji muhimu ndani ya kikosi cha kwanza cha Arsene Wenger.
Takwimu za soka zinaonyesha kuwa Walcott amefanya makubwa katika miaka yake 10 Gunner, huku kocha wake akiweka wazi kuwa nyota huyo amekuwa na mchango mkubwa katika mafanikio ya timu hiyo ya kaskazini mwa jiji la London.
Katika mechi 224 alizocheza kwenye kikosi cha Wenger, winga huyo amefunga magoli 53 na kutoa pasi za mwisho 41.
Takwimu hizo pia zinaonyesha kuwa Walcoth amecheza dakika 13,393 katika mechi zote 224 alizokitumikia Ligi Kuu kikosi cha mabingwa hao wa 2003/04 wa Ligi Kuu ya England.
Uwezo wake wa kukimbia kwa kasi na chenga za fedheha, umefanya awe mchezaji wa kutegemewa kwenye kikosi cha Arsenal na hata timu ya Taifa ya England, licha ya kukabiliwa na changamoto ya majeraha katika siku za karibuni.

Habari Kubwa