WALETE: Klopp awapangia mbinu mpya Arsenal leo

13Jan 2016
Lete Raha
WALETE: Klopp awapangia mbinu mpya Arsenal leo

KOCHA wa Liverpool, Jurgen Klopp, amesisitiza kuwa atalazimika kuwa na mbinu mpya ya kuifunga Arsenal leo licha ya kwamba ameshawakabili mara kadhaa akiwa na Borussia Dortmund.

Wachezji wa timu ya Arsenal

Klabu hiyo ya Bundesliga iliipiku Arsenal na kukaa kileleni mwa kundi lao la Ligi ya Mabingwa Ulaya katika misimu ya 2013-14 na 014-15, ingawa kikosi cha Arsene Wenger kiliwapiku katika msimu wa 2011-12.
Klopp, hata hivyo, amesisitiza kwamba michuano yake ya zamani dhidi ya Arsenal haitakuwa na maana yoyote katika mechi yao ya leo kwenye Uwanja wa Anfield na Mjerumani huyo amepongeza kazi kubwa aliyoifanya Arsene Wenger katika utawala wake London kaskazini.
"Hatupaswi kuzungumza sana kuhusu uzoefu wangu wa kucheza dhidi ya Arsenal," alisema katika mkutano na wanahabari kuelekea mechi yao ya leo.
"Tutatafuta mbinu mpya kwa ajili ya mechi hii. Jambo moja liko vilevile (kuhusu Arsenal), ni timu inayopiga soka tamu.
"Arsenal, pamoja na Man City, ndiyo timu bora kwenye Ligi Kuu ya England.
"Heshima yangu kwake (Wenger) inaongezeka siku hadi siku. Ni kazi ngumu sana kufanya kazi kwenye Ligi Kuu ya England na amekuwa akifanya kazi nzuri sana.
"Mechi dhidi ya Stoke ilikuwa ni ishara nzuri ya kitu gani timu yangu inaweza kufanya. Tunapaswa kukionyesha."
Klopp pia alibainisha kwamba Kolo Toure atakuwa fiti kuwavaa Arsenal leo, wakati pia beki wa kati, Mamadou Sakho (goti) pia anatarajiwa kurejea.
Jordon Ibe (misuli ya nyuma ya paja) na Jordan Henderson (mguu) pia wamerejea kikosini wakati Liverpool inayoshika nafasi ya nane katika msimamo ikianza kupungua.

AMKANA PATO
Klopp pia amekanusha ripoti zilizodai kuwa Liverpool wameingia maafikiano ya kumsajili Alexandre Pato kutoka Corinthians.

Habari Kubwa