Makocha kuwa na jazba kwa marefa zaidi ya wachezaji ni hatari
BAADA ya mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara kati ya Yanga na Kagera Sugar Jumatano iliyopita, Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam lilitokea tukio la kushangaza pale Kocha Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi, alipoingia uwanjani akitaka kumkunja mwamuzi wa pembeni wa mchezo huo.