Akiwasilisha Taarifa ya Utendaji kazi wa TAKUKURU, Mkurugenzi Mkuu wa taasisi hiyo, CP Salum Rashid Hamduni, amesema taasisi hiyo katika operesheni mbalimbali za kiuchunguzi imefanikiwa kuokoa bilioni 87.59 na uokoaji huo ulihusisha uokoaji wa dola za kimarekani milioni 33 sawa na shilingi bilioni 36.34
Kupitia uchunguzi wa mkongo wa taifa ambao ulibainika kuwa Umoja wa Watoa Huduma za Mawasiliono ulijenga miundombinu ya mawasiliano kinyeme na makubaliano na hivyo kuikosesha serikali mapato kutokana na huduma zao kutopita katika mkongo wa taifa.
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Charles Kichere, amesema mashirika ya Umma yanayojiendesha kibiashara yamepata hasara. Mwaka 2022/23, ATCL imepata hasara ya Tsh. Bilioni 56.64, sawa na ongezeko la 61% kutoka hasara ya Mwaka 2021/22 iliyokuwa Tsh. Bilioni 35.24. Ikumbukwe kuwa Shirika hili lilipokea ruzuku ya Tsh. Bilioni 31.55 kutoka Serikalini.
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Charles Kichere, amesema ukaguzi umebaini MSD ilitoa zabuni ya ununuzi wa vifaa vya maabara ambavyo ni vipimo vya COVID 19 kwa kampuni ambayo haikuwa mtengenezaji wa vifaa hivyo kinyume na makatwa ya zabuni, pia ilinunua vifaa hivyo bila kufuata ushauri, baada ya kufika kwa vifaa hivyo wataalamu walibaini havifai kwa matumizi yetu na tayari MSD ilikuwa imelipa fedha zote.
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (TAKUKURU), CP Salum Rashid Hamduni amesema walibaini Ongezeko la maombi ya Ubadilishwaji wa Matumizi ya Ardhi kutoka Matumizi ya awali na kuwa Matumizi ya Vituo vya Mafuta, huku tatizo la Ujenzi wa Vituo vya Mafuta katikati ya Makazi ya Watu likiongezeka na kuleta Changamoto ya Usalama wa Watu waishio karibu
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (TAKUKURU), CP Salum Rashid Hamduni amesema asilimia 79 ya Vituo vilivyochambuliwa vilizingatia Sheria kwa kuwa na vibali vya ujenzi kutoka halmashauri ambapo ujenzi umefanyika, asilimia 21 ya vituo havikuwa na leseni wakati zoezi la ufuatiliaji linafanyika.
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (TAKUKURU), CP Salum Rashid Hamduni, amesema walifanya uchambuzi kuhusu Mfumo wa Uzingatiaji wa taratibu za Ujenzi wa Vituo vya Mafuta katika Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani ambapo Vituo 38 vilihusika.
Kupitia mkataba wa makubaliano kati ya umoja wa watoa huduma za mawasiliono na wizara ya habari mawasiliono na teknolojia umoja huo ulikubali kulipa dola za kimarekani milioni 20 taslimu katika kipindi cha miaka mitano pamoja na riba ya asilimia 3.5.
© 2024 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED