Ni muhimu kudhibiti mianya ya ukwepaji, kuongeza walipakodi
RAIS Samia Suluhu Hassan juzi alizindua Tume ya Rais ya Kutathmini na Kushauri kuhusu Masuala ya Kodi na kubainisha kuwa mrejesho alioupata katika ukusanyaji wa kodi unaonesha kuwapo kwa malalamiko ya mianya ya ukwepaji wa kodi, makusanyo kidogo, huku mengi yakiingia mifukoni mwa watu.