Live updates

Prof. Mbarawa awasilisha vipaumbele vya bajeti Wizara ya Uchukuzi

Dotto Charles
Mwandishi
WAZIRI wa Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa.
PICHA: MAKTABA
WAZIRI wa Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa.
WAZIRI wa Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa amewasilisha bungeni makadirio ya mapato na matumizi ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2024/2025, jijini Dodoma leo, Mei 6, 2024, ambapo ameliomba Bunge kupitisha bajeti ya wizara hiyo ambayo ni zaidi ya shilingi trilioni 2.

Prof. Mbarawa, amesema katika kutekeleza Mpango na Bajeti kwa mwaka wa fedha 2024/25, Wizara hiyo itatumia kiasi cha shilingi 2, 729,676,417,000 kwa ajili ya matumizi ya kawaida na kutekeleza miradi ya maendeleo.

Amesema fedha hizo zitatumika katika miradi ya maendeleo ambayo ilikuwa tayari imeshaanzishwa ikiwa ni pamoja na kuendeleza ujenzi wa reli kwa kiwango cha kimataifa, kukarabati reli iliyopo katika MGR, kuendelea kuboresha na kuimarisha Shirika la ndege Tanzania (ATCL) na ukarabati wa meli katika maziwa makuu.

Ujenzi, ukarabati viwanja vya ndege vyatengewa bilioni 108.71

Dotto Charles
Mwandishi
news
PICHA: MAKTABA
Moja ya viwanja vya ndege nchini Tanzania.

“Ujenzi wa Kiwanja cha Arusha Shilingi bilioni 5.08, Ukarabati na Upanuzi wa Kiwanja cha Ndege cha Lindi Shilingi bilioni 13, Ukarabati na Upanuzi wa Kiwanja cha Ndege cha Moshi Shilingi bilioni 5, Ukarabati na Upanuzi wa Kiwanja cha Ndege cha Singida Shilingi bilioni.

“Upembuzi Yakinifu na Usanifu wa Kina wa Kiwanja cha Ndege cha Njombe kwa Daraja 4E. Shilingi milioni   692, Upembuzi Yakinifu na Usanifu wa Kiwanja kipya cha Ndege cha Kimataifa cha Serengeti Shilingi bilioni 1, Usanifu wa kina wa Jengo la Ofisi ya Makao Makuu ya TAA  Shilingi milioni 400.

“Ujenzi wa Kiwanja cha Mwanza Shilingi bilioni 15, Ujenzi wa Kiwanja cha Bukoba Shilingi bilioni 3.48, Ujenzi wa Kiwanja cha Mtwara Shilingi bilioni 7.3, Ukarabati wa kiwanja cha Ndege cha Kilimanjaro Shilingi bilioni 50, Uboreshaji na Upanuzi wa Jengo la Pili la Abiria JNIA Shilingi bilioni 6.08,”

Ujenzi, Ukarabati wa meli zatengewa bilioni 190.00

Dotto Charles
Mwandishi
news
PICHA: MAKTABA
Meli ya MV Mwanza.

Ujenzi wa Meli Ziwa Tanganyika

“Ujenzi wa meli mpya ya abiria 600 na mizigo tani 400 umetengewa Shilingi bilioni 25.

“Ujenzi wa meli mpya ya mizigo yenye uwezo wa kubeba tani 3,500 Shilingi bilioni 35.

“Kujenga kiwanda cha kujengea Meli chenye uwezo wa kubeba meli zenye uzito wa tani 5,000 Shilingi bilioni 30.

“Ujenzi wa meli mpya ya mizigo yenye uwezo wa kubeba tani 3,000 Shilingi bilioni 20,”

 Ukarabati katika Ziwa Tanganyika

“Ukarabati wa meli ya MV Liemba Shilingi bilioni 5, Ukarabati wa meli ya mafuta ya MT Sangara Shilingi bilioni 1.5, “Ukarabati wa meli ya MV Mwongozo Shilingi milioni 300,”

ATCL yatengewa bilioni 324.5

Dotto Charles
Mwandishi
news
PICHA: MAKTABA
Ndege ya ATCL.

Kuendelea kuboresha na kuimarisha Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) kwa kununua ndege tatu (3), vipuri, injini na kukarabati miundombinu wezeshi. Shilingi bilioni 324.5 zimetengwa.

Ujenzi reli ya SGR watengewa trilioni 1.511

Dotto Charles
Mwandishi
news
PICHA: MAKTABA
Mafundi wakiwa kwenye mwendelezo wa ujenzi wa reli.

Waziri Mbarawa ametaja miradi hiyo ya Maendeleo inayoendelea na kiasi cha fedha zilizotengwa kwa ajili ya utekelezaji huo:

“Kuendeleza ujenzi wa reli kwa kiwango cha kimataifa (Standard Gauge Railway - SGR) katika maeneo yaliyobaki pamoja na ununuzi wa vitendea kazi (vicha na mabehewa) ambapo jumla ya Shilingi trilioni 1.511 zimetengwa.

“Kufufua Reli ya MGR kipande cha Kilosa – Kidatu Kilomita 108 ambapo kimetengwa kiasi cha Shilingi bilioni 1. Ukarabati wa Reli iliyopo katika ya MGR  Shilingi bilioni 312.03 zimetengwa.