Live updates

Watu saba wafariki ajalini Singida, basi la Lujiga Express likigonga lori

Thobias Mwanakatwe
Mwandishi
Ajali ya basi la Luginga Express lililogonga lori.
Picha: Tobias Mwanakatwe
Ajali ya basi la Luginga Express lililogonga lori.
WATU saba wamefariki dunia papo hapo na wengine zaidi ya 15 kujeruhiwa baadhi yao vibaya baada ya basi la Kampuni ya Lujiga Express walilokuwa wakisafiria kutoka Dar es Salaam kwenda Mwanza kugonga lori la mizigo kwa nyuma ambalo lilikuwa limeegeshwa barabarani kutokana na kuharibika.

Mkuu wa Wilaya ya Iramba mkoani Singida, Suleiman Mwenda,akizungumza na Nipashe Digital hili Leo kwa njia simu amesema ajali hiyo imetokea Leo saa 10:30 alfajiri katika kijiji cha Malendi kilichopo kata ya Mgongo wilayani humo.

Taarifa ya Polisi Singida, ajali ya basi na lori iliyoua watu 9

Thobias Mwanakatwe
Mwandishi
Ajali ya basi la Lujiga Express na lori.

Waliokufa wafikia 9, Majeruhi mjamzito afanyiwa upasuaji mtoto afariki tumboni

news
Picha: Thobias Mwanakatwe
Ajali ya basi la Lujiga Express lenye namba za usajili T 315 CXX na Lori.

IDADI ya watu waliokufa katika ajali ya basi la Lujiga Express  lenye namba za usajili T 315 CXX iliyotokea wilayani Iramba mkoani Singida imefikia 9 na majeruhi 19.

Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Daniel Paul. amesema kati ya majeruhi hao , watatu ambao walikuwa wamelazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Iramba (Kiomboi) alikuwepo mwanamke mjamzito ambaye amefanyiwa operesheni na mtoto kukutwa amefariki tumboni.

Hivi ndivyo basi la Lujiga Express lilivyogonga Lori na kusababisha vifo vya watu saba

Thobias Mwanakatwe
Mwandishi
Basi la Lujiga lililogonga lori.