Live updates

Waziri Aweso awasilisha bungeni bajeti ya Wizara ya Maji

Frank Monyo
Mwandishi
Waziri wa Jumaa Aweso.
Picha: Bunge
Waziri wa Jumaa Aweso.
Waziri wa maji, Jumaa Aweso leo amewasilisha makadirio ya bajeti ya wizara hiyo.

"Wizara kwa kushirikiana na wadau imeanza kuandaa Mpango Kabambe wa Taifa wa Maji katika mikoa ya Rukwa, Dodoma na Njombe na zoezi hilo litaendelea katika mikoa mingine iliyobakia katika mwaka 2024/25"- Waziri Aweso 

Aweso aliomba Bunge kupitisha Sh. bilioni 627.7 bajeti Wizara ya Maji

Frank Monyo
Mwandishi
news
Picha: Bunge.
Waziri wa Maji, Jumaa Aweso.

Waziri wa Maji, Jumaa Aweso akiwasilisha bungeni makadirio ya mapato na matumizi ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2024 / 25, jijini Dodoma leo Mei 9, 2024. Aweso ameliomba bunge lipitishe bajeti ya wizara yake kiasi cha Sh. bilioni 627. 7.

Rais Samia hapatikani kila mahali, wabunge tumempata tumtumie

Frank Monyo
Mwandishi
news
Picha: Mtandaoni
Rais Samia Suluhu Hassan akizungumza jambo na Waziri wa Maji Jumaa Aweso katika moja ya mikutano.

"Katika bajeti hii ukiachana na miradi ambayo tutakwenda kuipitisha, Rais Samia Suluhu Hassan  ametoa zawadi maalum kwa kila mbunge wa jimbo anakwenda kuchimba visima vitano katika maeneo ya mijini na vijijini mahali ambapo mbunge unaona kuna changamoto ya maji, Rais Samia hapatikani kila mahali na hapatikani kila wakati, wabunge tumempata lazima tumtumie kwa maslahi ya Watanzania na itoshe kusema Dkt Samia ni suluhu kwa matatizo ya Watanzania, " - Waziri wa Maji Jumaa Aweso

Maji yanayosambwaza mjini, vijijini yanakidhi viwango

Frank Monyo
Mwandishi
news
Picha: Mtandaoni.
Maji kwenye bomba.

"Takwimu zinaonesha kuwa hali ya ubora wa maji kwenye vyanzo vya maji juu na chini ya ardhi inawezesha ustawi wa ikolojia na hivyo vinaweza kuendelezwa kwa matumizi ya sekta mbalimbali lakini bado kunahitajika jitihada za kuzuia uchafuzi, kurejesha na kuimarisha ubora wa maji kwenye vyanzo," - Waziri wa Maji, Jumaa Aweso 

"Maji yanayosambazwa vijijini na mijini yameendelea kukidhi viwango vya kitaifa vya ubora wa maji ya kwa matumizi ya kunywa na kupikia pamoja na shughuli mbalimbali za kiuchumi," - Waziri wa Maji Jumaa Aweso

Utoaji huduma ya maji safi vijijini umeimarika

Frank Monyo
Mwandishi
news
Picha: Mtandaoni
Huduma ya maji safi kijijini.

Waziri wa Maji Jumaa Aweso amesema huduma ya majisafi na salama vijijini na mijini imeimarika, ambapo kwa upande wa Vijijini wastani umeongezeka kutoka wastani wa 77% Desemba 2022 hadi 79.6 Desemba, 2023 na mijini kutoka wastani wa 88% Desemba, 2022 hadi 90% Desemba, 2023.

Hivi hapa vipaumbele 10 vya Wizara ya Maji

Frank Monyo
Mwandishi
news
Picha: Bunge
Waziri wa Maji, Jumaa Aweso.

Waziri wa Maji, Jumaa Aweso amesema Wizara imeweka vipaumbele ambavyo vitazingatiwa katika mpango na bajeti ya mwaka 2024/25 ili kufikia lengo la kuwapatia huduma ya maji safi na salama kwa zaidi ya asilimia 85 ya wananchi wa vijijini na zaidi ya asilimia 95 ya wakazi wa mijini.

Vipaumbele hivyo ni kama ifuatavyo:-

1. Kuendelea na usimamizi na uendelezaji wa rasilimali za maji

2. Kukamilisha utekelezaji wa miradi inayoendelea na kuendelea na ujenzi wa miradi mikubwa

3. Kuendelea kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi kwa kuongeza kasi ya uvunaji wa maji ya mvua kupitia ujenzi wa mabwawa ya ukubwa wa kati na mabwawa ya kimkakati kwa kushirikiana na Sekta za Mifugo, Kilimo, Utalii na Mazingira

4. Kuimarisha matumizi ya mitambo ya uchimbaji wa visima na mabwawa iliyonunuliwa ili kufikisha huduma ya maji kwenye vijiji ambavyo havina huduma ikiwa ni pamoja na kutekeleza Programu ya kuchimba visima 900 na ujenzi wa mabwawa madogo madogo

5. Kukamilisha uandaaji wa Mpango Kabambe wa Taifa wa Maji (Water Master Plan), Mtandao wa Taifa wa Kusambaza Maji (National Water Grid) na kukamilisha mapitio ya Sera ya Taifa ya Maji ya mwaka 2002

6. Kupunguza upotevu wa maji kwa kuendelea kukarabati miundombinu chakavu, kufunga mifumo ya kuweza kutambua maeneo yenye mivujo (ILMS) na kushirikisha viongozi wa Serikali za Mitaa kwa ajili ya kutoa taarifa za upotevu wa maji kwa wakati

7. Kuongeza kasi ya ufungaji wa dira za malipo kabla ya matumizi ya maji (prepaid meters) ili kuongeza makusanyo na kupunguza malalamiko ya wateja

8. Kuongeza kasi ya uwekezaji wa miundombinu ya uondoshaji majitaka kwenye Miji Mikuu ya Mikoa na Wilaya

9. Kuimarisha utoaji wa huduma bora ya majisafi kupitia Mamlaka za Maji na Usafi wa Mazingira na CBWSOs kwenye eneo la maunganisho ya wateja wapya na kuhakikisha masaa ya upatikanaji wa huduma ya maji yanaongezeka

10. Kuongeza ushiriki wa sekta binafsi katika uwekezaji na uendeshaji wa miradi na skimu za maji.

Miradi 1,054 ya usambazaji maji vijijini kutekelezwa

Frank Monyo
Mwandishi
news
Picha: Mtandaoni
Usambazaji wa huduma ya maji vijijini.

"Katika mwaka 2024/25, Wizara imepanga kuendelea kutekeleza jumla ya miradi 1,054 ya usambazaji maji vijijini katika maeneo mbalimbali ikiwemo maeneo yanayozunguka vyanzo vya Bwawa la Kidunda na vijiji vilivyopitiwa na mradi wa Same Mwanga. Aidha, kuendelea kuhamasisha ushiriki wa sekta binafsi katika utoaji wa huduma ya maji, kuzijengea uwezo CBWSOs ili kuimarisha uwezo wa kujiendesha"- Jumaa Aweso, Waziri wa Maji

Mwaka 2024)25 ujenzi Bwawa la Kidunda, Farkwa kuendelea

Frank Monyo
Mwandishi
news
Picha: Mtandaoni
Bwawa Kidunda

"Katika mwaka 2024/25, Serikali imepanga kuendelea na ujenzi wa bwawa la kimkakati la Kidunda na kuanza mradi wa ujenzi wa bwawa la Farkwa; kukarabati mabwawa 19 na kuendelea na ujenzi wa mabwawa 25 ya ukubwa wa kati na mdogo; na kufanya usanifu wa mabwawa 45."-Jumaa Aweso, Waziri wa Maji

Miaka mitatu ya Rais Samia, visima 283 vimechimbwa

Frank Monyo
Mwandishi
news
Picha: Maktaba
Gari maalumu la kuchimba visima likiwa kazini.

""Katika Kipindi cha Utekelezaji wa Bajeti 2023 /2024 chini ya uongozi wa Rais Samia Sekta ya Maji imepata mafanikio makubwa yafuatayo Kuongezeka kwa ufanisi katika uchimbaji wa visima na ujenzi wa mabwawa kwa kutumia mitambo iliyonunuliwa na Serikali ya Awamu ya Sita ya Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo jumla ya visima 283 vimechimbwa. Aidha, mitambo hiyo imesaidia kukabiliana na janga la maafa la Hanang’ mkoani Manyara kwa kuchimba visima nane (8) na kukarabati Bwawa la Nanja; na kuchimba visima sita (6) vinavyohudumia wananchi katika eneo la Msomera"- Jumaa Aweso, Waziri wa Maji

Gridi ya Taifa ya Maji inakuja-Aweso

Frank Monyo
Mwandishi
news
Picha: Bunge
Jumaa Aweso Waziri wa Maji

"Katika Kipindi cha Utekelezaji wa Bajeti 2023 /2024 chini ya uongozi wa Rais Samia Sekta ya Maji imepata mafanikio makubwa yafuatayokuanza kwa utekelezaji wa mpango wa kuwa na Gridi ya Taifa ya Maji kwa kutumia vyanzo vikubwa vya maji ikiwemo maziwa, mito na mabwawa kupeleka maji maeneo yasiyo na vyanzo vya uhakika"-Jumaa Aweso Waziri wa Maji

Tanga UWASA, taasisi ya kwanza Afrika Mashariki kuingia Soko la Hisa

Frank Monyo
Mwandishi
news
Picha: Mtandaoni
Ofisi za Tanga UWASA.

"Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Tanga imekuwa Taasisi ya kwanza Tanzania na Afrika Mashariki kuingia katika Soko la Hisa na imepata fedha Shilingi Bilioni 54.72 sawa na asilimia 103. Narudia, imevunja rekodi ya kuwa Taasisi ya kwanza Tanzania na Afrika Mashariki. Huu ni ubunifu na udhubutu mkubwa. Tunawashukuru Watanzania na Waheshimiwa Wabunge kwa kununua hisa za Mamlaka ya Maji Tanga. Hili ni funzo kuwa, It can be done, play your part.-Jumaa Aweso Waziri wa Maji

Hizi ni LUKU za maji. Hii ndio Dunia ya kisasa- Aweso

Frank Monyo
Mwandishi
news
Picha: Mtandaoni
Dira ya malipo kabla ya matumizi.

"Hili ni agizo la Mama Samia kwa Wizara ya Maji. Nasi tunamhakikishia Mama kupitia Ezra 10:4 kuwa kazi tunaiweza natimu ya Wizara iko imara kuitenda kwa uaminifu. Naomba Waheshimiwa Wabunge tuhamasishe wananchi kufunga dira za malipo kabla ya matumizi. Hizi ni LUKU za maji. Hii ndio Dunia ya kisasa na huu ndio mwelekeo. Napenda kumuahidi Mheshimiwa Rais, kuwa lugha yetu ni pre - paid meters, na maono yetu ni kuwa na viwanda vya pre paid meters"- Jumaa Aweso
Waziri wa Maji

Aweso : Wizara yaandaa mkakati kasi ufungaji 'Pre-paid meters'

Frank Monyo
Mwandishi
news
Picha: Bunge
Jumaa Aweso Waziri wa Maji.

"Mnamo tarehe 4 Machi, 2024, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan aliielekeza Wizara ya Maji kuongeza kasi ya ufungaji wa dira za maji za malipo kabla ili kuwafikia wananchi wote nchini. Katika kutekeleza agizo hilo, Wizara imeandaa Mkakati wa Kuongeza Kasi ya Ufungaji wa Dira za Maji za Malipo Kabla ambapo kupitia Mkakati huo asilimia 50 ya wateja wa maji vijijini na mijini watafungiwa dira hizo ifikapo Desemba 2025"- Jumaa Aweso
Waziri wa Maji.

Wateja 13,526 wamefungiwa dira za maji za malipo kabla

Frank Monyo
Mwandishi
news
Picha: Mtandaoni
Pre-paid water meters.

"Wizara imeanza kutumia teknolojia ya matumizi ya dira za maji za malipo kabla (pre-paid water meters) kwa lengo la kupunguza maji yanayopotea na malalamiko yanayohusiana na ankara za maji. Hadi mwezi Aprili 2024, jumla ya wateja 13,526 katika maeneo ya vijijini na mijini wamefungiwa dira hizo zikiwemo Mamlaka za Maji za Iringa ambayo imefunga dira 6,544, Dodoma (1,085) na Mamlaka ya Maji Tanga dira 627. Kwa upande wa vijijini, RUWASA imewafungia dira hizo wateja 1,846 kwenye mikoa mbalimbali"-Jumaa Aweso Waziri wa Maji

Maziwa ya Tanganyika, Nyasa na Victoria yana maji 25% yote matamu

Frank Monyo
Mwandishi
news
Picha: Mtandaoni
Ziwa Tanganyika.

"Waheshimiwa Wabunge wa Majimbo yaliyo katika mwambao wa Maziwa ya Tanganyika, Nyasa na Victoria pamoja na maeneo kame, mtoto wenu National Water Grid karibu anazaliwa. Maziwa ya Tanganyika, Nyasa na Victoria yana asilimia 25 ya maji yote matamu duniani, hivyo maono hayo makubwa ya Mama Samia lazima tuyatekeleze. Na sisi Wizara ya Maji, hatutakuwa kikwazo. Narudia, Mradi wa National Water Grid ni maono makubwa ya Taifa linalojiamini na kuthubutu. Taifa hilo ni Tanzania chini ya Mama Samia"- Jumaa Aweso Waziri wa Maji