Mamia wapinga uwepo wa Jeshi la Marekani nchini Niger

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 04:55 PM Apr 22 2024
Maandamamno ya mjini Niamey kupinga uwepo wa wanajeshi wa Marekani.
Picha: Mahamadou Hamidou/REUTERS
Maandamamno ya mjini Niamey kupinga uwepo wa wanajeshi wa Marekani.

MAMIA ya watu wameandamana ili kupinga uwepo wa wanajeshi wa Marekani nchini Niger, huku ujumbe kutoka Washington ukitarajiwa kuwasili nchini humo siku chache zijazo ili kupanga mikakati ya kujiondoa katika taifa hilo linalotawaliwa na jeshi.

Marekani imekubali kuondoa wanajeshi wake zaidi ya 1,000 kutoka katika taifa hilo la Afrika ambalo Washington ilijenga kambi yenye thamani ya dola milioni 100 kwa ajili ya kurusha ndege zisizokuwa na rubani. 

Maandamano hayo yalifanyika katika mji wa kaskazini wa jangwa wa Agadez ambapo kuna makazi ya kituo cha jeshi la anga la Marekani, na yaliitishwa na muungano wa kundi la vyama 24 vya kiraia ambavyo vinauunga mkono utawala wa jeshi tangu mapinduzi ya mwaka jana.