Marekani yaanza kuondoa wanajeshi wake nchini Niger

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 07:36 AM May 20 2024
Sehemu ya wanajeshi wa Marekani waliopo nchini Niger.
Picha: Alex Fox Echols Iii/Planetpix/ZUMAPRESS.com/picture alliance
Sehemu ya wanajeshi wa Marekani waliopo nchini Niger.

SERIKALI ya Marekani imeanza kuondoa wanajeshi wake kutoka Niger baada ya kuombwa kufanya hivyo na watawala wa kijeshi wa taifa hilo la Afrika Magharibi.

Tangazo la kuanza kuondoka wanajeshi hao limetolewa mapema leo hii kwa pamoja na nchi hizo mbili. 

Taarifa hiyo imesema zoezi hilo linatarajiwa kukamilika kabla ya Septemba 15. Pande hizo zilitangaza kufikia makubaliano ya kuondolewa wanajeshi hao waliopelekwa kuisaidia Niger kupambana na makundi ya itikadi kali za dini.

Utawala mpya wa kijeshi ulioipindua serikali ya kidemokrasia katikati mwa mwaka jana umesema wanajeshi hao wa Marekani walikuwemo nchini Niger kinyume cha sheria.

DW imeandika kuwa, Askari wa Marekani takriban 650 wapo nchini Niger pamoja na kambi kubwa ya drone karibu na mji wa kaskazini mwa Taifa hilo Agadez.