Waziri Mkuu wa Slovakia apigwa risasi tumboni

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 07:14 AM May 16 2024
Waziri Mkuu wa Slovakia, Robert Fico.
Picha: Petr David Josek/AP Photo/picture alliance
Waziri Mkuu wa Slovakia, Robert Fico.

WAZIRI Mkuu wa Slovakia, Robert Fico amepigwa risasi na kujeruhiwa tumboni muda mfupi baada ya kumaliza kuongoza kikao cha Baraza la Mawaziri.

Duru kutoka nchini humo zinasema shambulio hilo limetokea kwenye mji wa Handlova ulio kiasi kilometa 190 kaskazini magharibi mwa Mji Mkuu Bratislava.

Kiongozi huyo tayari amekimbizwa hospitali kwa matibabu na anayedaiwa kutenda tukio hilo tayari amekamatwa. Polisi ililazimika kuwaondoa watu kwenye kituo cha utamaduni ambako kikao hicho kilikuwa kinafanyika.

Salamu za pole zimeanza kumiminika kutoka kwa viongozi barani Ulaya wengi wakilaani mkasa huo.

Rais Zuzana Caputova wa Slovakia amesema ameshtushwa na shambulio hilo alilolitaja kuwa la kikatili na amemtakia Fico afua ya mapema. Viongozi wengine akiwemo kansela Olaf Scholz wa Ujerumani, Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak na marais wawili wa Umoja wa Ulaya wamelaani kisa hicho.