FABIAN Pauline mkazi wa kata ya Malya wilayani Kwimba mkoani Mwanza, amemshambulia kwa fimbo na kumsababishia kifo mtoto wake aitwaye Alvin Fabian mwenye umri wa miaka mitatu baada ya kumkuta amejichafua na kinyesi baada ya kujisaidia.
Akizungumzia tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza DCP Wilibroad Mutafungwa amesema mtuhumiwa huyo ambaye ndiye Baba mzazi wa mtoto huyo, alimkuta mtoto wake akiwa amejipaka kinyesi mwili mzima ndipo alimshambulia kwa fimbo katika maeneo mbalimbali ya mwili wake na kupelekea kifo hicho.
Hata hivyo baada ya kufanya kitendo hicho, Jeshi la Polisi mkoani humo lilifanikiwa kumtia mbaroni ambapo taratibu za kisheria zinaendelea ipi afikishwe mahakamani.
Aidha katika tukio lingine, mtoto mwingine mwenye umri wa miaka nane na mwanafunzi wa darasa la kwanza huko katika kata ya Kisesa wilayani Magu, amejeruhiwa vibaya kwa kupigwa na ubapa wa panga, fimbo na mkanda wa suruali na baba yake mzazi aitwaye Ezron Macheya, kwa madai kuwa mtoto huyo amekuwa akirudi nyumbani amechelewa.
© 2024 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED