Chikota aomba serikali kutatua uhaba wa walimu, watumishi wa afya Nanyamba

By Augusta Njoji , Nipashe
Published at 03:51 PM Apr 17 2024
Mbunge wa Jimbo la Nanyamba Abdallah Chikota.
Picha: Mpigapicha Wetu
Mbunge wa Jimbo la Nanyamba Abdallah Chikota.

Mbunge wa Jimbo la Nanyamba Abdallah Chikota amesema mahitaji wa watumishi wa sekta ya afya Mkoa wa Mtwara ni 6,088 na waliopo ni 2,153 ambapo upungufu ni asilimia 65.

Aidha, amesema kuna upungufu mkubwa walimu  na kushauri TAMISEMI kuhakikisha inatoa kibali cha walimu 300 kuajiriwa katika Halmashauri ya Nanyamba.

Pia, amependekeza kuwa TAMISEMI ipewe kibali maalum cha kuajiri Wahandisi wa barabara kwaajili ya kupelekwa wilayani.

Akichangia makadirio ya mapato na matumizi ya  Ofisi ya Rais TAMISEMI 2024/25 bungeni, Chikota pamoja na ombi hilo, 
amempongeza  Rais  Samia Suluhu Hassan kwa kuanzisha kongani ya viwanda vya kubangua korosho mkoani Mtwara ambayo imesaidia  uzalishaji wa ajira.

“Tunamshukuru Rais kwa mradi wa umwagiliaji wa Arusha chini, ujenzi wa viyuo vya afya vitatu, mradi wa TACTIC, ujenzi wa stendi mpya ya mabasi na ujenzi wa barabara ya lami kilomita tano,” amesema Chikota.