MKUU wa Wilaya ya Ludeva mkoani Njombe, Victoria Mwanziva amesema kampeni ya msaada wa kisheria ya Mama Samia ‘Mama Samia Legal Aid Campaign’ imeanza rasmi jana na itafikia mwisho Juni 4, 2024 wilayani humo.
DC Mwanziva amesema kampeni hiyo inalenga kutoa elimu ya masuala ya kisheria kuhusu ardhi, madai, mirathi, ndoa, jinai, haki za binadamu, utawala bora na utatuzi wa migogoro kwa njia mbadala.
Amesema kampeni hiyo itatoa huduma ya msaada wa kisheria kwa Wananchi pamoja na ufanya uwakilishi wa wananchi wasio na uwezo mahakamani hata hivyo amesema kampeni inalenga pia kujenga uwezo mabaraza ya usuluhishi ya kata, kujenga uwezo wa maofisa wa serikali, watendaji wa vijiji na kata.
“Ludewa tunamshukuru Mheshimiwa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kampeni hii ya kitaifa, wataalam wa kisheria kutoka Wizara ya Katiba na Sheria wapo Ludewa na sisi Wilaya ya Ludewa tumeipokea kampeni hii kwa mikono miwili na kazi inaendelea Ludewa,” amesema DC Mwanziva
© 2024 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED