Kilombero Sugar yazindua kampeni ya ushirikishaji wakulima na uwekezaji

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 04:09 PM Jun 21 2024
Kilombero Sugar yazindua kampeni ya ushirikishaji wakulima na uwekezaji.
Picha:Mpigapicha Wetu
Kilombero Sugar yazindua kampeni ya ushirikishaji wakulima na uwekezaji.

Kampuni ya Kilombero Sugar imetangaza uzinduzi wa kampeni ya ushirikishaji wakulima na uwekezaji kama sehemu ya mradi wake wa kupanua kiwanda cha K4.

Kauli mbiu ya Kampeni hiyo ni "Soko la kuaminika, kipato endelevu, na kuboresha maisha,"  ambapo inalenga kuimarisha maendeleo miongoni mwa wakulima wa miwa kupitia mawasiliano ya kimkakati na ushirikiano na wadau.

Kampeni hiyo imezinduliwa rasmi katika mashamba ya miwa ya Kilombero na imefanikiwa kuhudhuriwa na watu wengi, ikijumuisha ushiriki wa wasimamizi, maafisa wa serikali za mitaa, na wakulima wa miwa, ambao wote ni viungo  muhimu katika mnyororo wa thamani wa kilimo cha miwa.

Kutokana na changamoto za msimu uliopita zilizosababishwa na mvua kubwa zilizopelekea El-Nino, Kilombero Sugar imechukua hatua madhubuti ya kuwatuliza na kuwaliwaza wakulima kupitia mradi wa wa upanuzi wa kiwanda cha K4.

Ambao hadi sasa umefikia 90%, Huu ni uwekezaji mkubwa kuwahi kufanywa na illovo barani Afrika. Mradi huu mkubwa unathibitisha imani ya kampuni kwa jamii ya wakulima wa ndani, ambao watazalisha 60% ya miwa inayohitajika katika kiwanda hicho.

 Akizungumza katika hafla hiyo, Pierre Redinger ambaye ni Mkurugenzi wa Wakulima wa nje Kilombero Sugar, amesisitiza jukumu muhimu la jamii katika jitihada hizi  nakueleza kuwa.. “Uwekezaji wetu katika Mradi wa Kupanua kiwanda cha K4 unatokana na imani tuliyonayo kwa wakulima wetu, safari hii ilianza mwaka 2018 kwa usajili wa wakulima, ukiungwa mkono na Ofisi ya Wilaya ya Kilombero, ambao ulifungua njia kwa biashara hii muhimu."

Redinger pia alitangaza kuwa Kilombero Sugar imejitolea kutoa mkopo wa mbegu za miwa tani 20000 kwa wakulima, kwa msimu wa upandaji wa 2024/25 na 2025/26, ambao utasaidia zaidi upanuzi huo.

George Gowelle, ambaye amemuwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Sukari Tanzania, ameelezea mchango mkubwa wa serikali katika mradi huu, akisema kuwa serikali itaendelea kuunga mkono juhudi zinazolenga kuongeza utoshelevu wa sukari. Anaongeza kuwa. "Kilombero Sugar imeweka mfano wa kuigwa, na serikali itaendelea kuunga mkono jitihada kama hizi." 

Bakari  Mkangama, Mwenyekiti wa Kilombero Joint Enterprises Cooperatives Society, inayowakilisha AMCOS 17 zinazofanya kazi moja kwa moja na Kilombero Sugar, ameisifu  kampeni hiyo kama fursa ya mabadiliko.

 "Mpango huu utaleta mabadiliko makubwa kwa soko letu la kuaminika, kipato endelevu, na kuboresha maisha," alisema  Mkangama. nakuomngeza kuwa: "Tunapaswa kuchangamkia fursa hii adhimu."Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kilombero, Dunstan Kyobya, amepongeza juhudi  za Kilombero Sugar. "Mpango huu wa Kupanua kiwanda cha  K4 na kampeni ya Kuinua Wakulima ni jambo muhimu kwa kipato endelevu kitakachoboresha maisha ya wakulima wa miwa katika Bonde la Kilombero," alisema Kyobya na kuongeza kuwa;

 "Serikali imejitolea kuunda mazingira mazuri kwa uwekezaji wa biashara na ustawi wa jamii."

 Kilombero Sugar, kupitia kampeni ya Kuinua Wakulima, inathibitisha tena kujitolea kwake katika kuwekeza kwa watu, mafunzo, na teknolojia, kuweka kiwango kipya cha kilimo nchini Tanzania.