Mkurugenzi ATE ataka mjadala matumizi Akili Mnemba

By Frank Monyo , Nipashe
Published at 01:21 PM Jun 21 2024
Mkurugenzi Mtendaji wa ATE, Suzanne Ndomba-Doran.

Mkurugenzi Mtendaji wa ATE, Suzanne Ndomba-Doran, amesema matumizi ya Akili Mnemba yameleta mashaka kidogo ya kwamba inaweza kufanya kazi mbalimbali na kusababisha ukosefu wa ajira.

Aidha amesema kuwa ni vigumu kufahamu jinsi gani akili bandia itaweza kuathiri kazi siku zijazo lakini ni vema kama nchi kuanza kujadili mabadiliko haya. 

Kauli hiyo ameitoa jana wakati akitoa salamu za utangulizi katika Mkutano Mkuu wa mwaka wa ATE, uliobeba dhima ya "Afya ya akili katika ulimwengu wa kidijitali."

Alisema maendeleo ya teknokojojia huacha makundi mengine nyuma hivyo ni vyema katika mijadala hii makundi mbalimbali yakahusishwa ili kuweza kuendana na kasi hiyo. 

Alisema kuwa mambo mengi mazuri yanaletwa na teknolojia na yapo mambo hasi ambayo yatatokana na jinsi tunavyotumia teknolojia. "Matumizi mabaya ya teknolojia yanaweza kuleta wasiwasi, msongo wa mawazo,kuathiri Maisha na utendaji wa kazi. Pia maendeleo ya teknolojia huleta changamoto ya afya ya akili, leo tutajadili juu ya afya ya akili katika ulimwengu wa teknolojia, ili kuhakikisha maeneo ya kazi ni salama na yenye afya" alisema 

Wito Kwa waajili kuendelea kutumia huduma za online zinazotolewa na WCF ili kuwapunguzia gharama, pia mapinduzi hayo ya huduma za online ni muendelezo wa mapinduzi ya huduma za kidigitali ambayo Dunia mzima inapitia ikiwemo Tanzania.Dk. John Mduma, Mkurugenzi WCF

Aliongeza kuwa maendeleo ya teknokojojia huacha makundi mengine nyuma hivyo ni vyema katika mijadala hii makundi mbalimbali yakahusishwa ili kuweza kuenda katika kasi hiyo.

"Napenda kutumia nafasi hii kuwakumbusha Waajiri kuendelea kutoa kipaumbele kwenye suala la Afya ya Akili katika maeneo yao ya kazi na kuzingatia sera za Afya na Usalama.
Kupitia mjadala huu itakuwa ni mwanzo mzuri wa kujua ni namna gani katika ulimwengu wa Kazi tumejipanga kuendana ma Mabadiliko haya sambamba na kuangalia fursa na changamoto zitakazojitokeza pamoja na kutoa mapendekezo. ~ Hery Mkunda, Katibu TUCTA.
Sisi ATE tukiwa ndio wawakilishi wa Waajiri nchini tumekuwa tukihamasisha na kuwashauri waajiri nchini kuweka Sera na miongozo mbalimbali zitakazosaidia kuboresha Afya ya Akili kazini" alisema 

Alisema kuwa muongozo wa pamoja wa Shirika la Kazi Duniani (ILO) na Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) wa mwaka 2022 umependekeza hatua za kuchukuliwa ili kukabiliana na changamoto za afya ya akili katika maeneo ya kazi.
Afya ya akili imekuwa ikijitokeza na kuwagusa watu katika maeneo ya kazi na hata kuathiri utendaji kazi. Nitoe rai kwa waajiri nchini kuweka program zitakazosaidia kuimarisha afya ya akili kwa wafanyakazi ili kuongeza tija sehemu za kazi.-Hery Mkunda, Katibu TUCTA