Mradi wa machimbo ya dhahabu Nyanzaga kuanza

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 05:00 PM Apr 19 2024
Waziri wa Madini Anthony Mavunde akizungumza na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Perseus ya Australia Jaffer Quartamaine.
Picha: Mpigapicha Wetu
Waziri wa Madini Anthony Mavunde akizungumza na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Perseus ya Australia Jaffer Quartamaine.

Waziri wa Madini Anthony Mavunde leo amefanya kikao cha pamoja na Kampuni ya Perseus ya Australia ikiongozwa na Mtendaji Mkuu wake Jaffer Quartamaine juu ya uendelezwaji wa mradi wa Nyanzaga unaomilikiwa kwa ubia kati ya Serikali ya Tanzania na Kampuni ya Ore Corp ambayo hisa zake zimenunuliwa na Kampuni ya Perseus.

Katika kikao hicho, Waziri Mavunde ameipongeza Kampuni ya Perseus kwa kufanikiwa kukamilisha wa mchakato wa ununuzi wa hisa za Kampuni ya Ore Corp na kuitaka Kampuni hiyo kukamilisha kwa uharaka malipo ya fidia kwa wananchi wanaopisha mradi.

Pia Waziri Mavunde amewataka wawekezaji hao kuhakikisha wanaanza mapema uendelezaji wa mradi kwa mujibu ya makubaliano ya awali ya kimkataba ili nchi ianze kunufaika na matunda ya utekelezaji wa mradi huu mkubwa wa dhahabu katika Wilaya ya Sengerema,Mkoa wa Mwanza.

Akizungumza katika kikao hicho,Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Perseus  Jaffer Quartamaine*ameishukuru serikali ya Tanzania kwa ushirikiano mkubwa wakati wote wa mchakato wa ununuzi wa hisa za Kampuni ya Ore Corp na kuahidi kwamba wamejipanga kuanza uendelezaji wa mradi huu mapema kadri iwezekanavyo kutokana na mpangilio wa utekelezaji wa shughuli mbalimbali za utekelezaji wa mradi.