Nyumba zaidi ya 2,000 zimezingirwa na maji Karatu

By Getrude Mpezya , Nipashe
Published at 09:19 PM Apr 22 2024
Nyumba zilizozingirwa na maji Karatu.
Picha: Getrude Mpezya
Nyumba zilizozingirwa na maji Karatu.

Makazi ya Wananchi zaidi ya 2,000 wilayani Karatu Mkoa wa Arusha yakiwa yamejaa maji baada ya Bwawa linalopokea maji kutoka katika Milima ya Ngorongoro kujaa maji yaliyopelekea kuingia kwenye makazi ya watu kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha mfululizo.

Wakizungumza na waandishi wa habari wananchi hao wamesema kuwa kujaa kwa maji hayo katika maeneo yao ni kutokana na bwawa linalopokea maji yanayotoka katika milima ya Ngorongoro kujaa uchafu unaotoka katika maeneo mbalimbali ya karatu ambapo imepelekea bwawa hilo kufurika na kusababisha maji kujaa katika nyumba za wakazi wa eneo hilo la bwawani.

Naye Mbunge wa Karatu Mjini, Daniel Awack amewapa pole wananchi hao baada ya kutembelea makazi yao na kuiomba Serikali kuwapatia msaada wa dharura wa chakula na mahali pa kuishi wakazi wa kata ya karatu huku yeye akitoa zaidi ya gunia 200 za mahindi iliwaweze kugawana kwa kila mmoja haswa kwa wale waliokosa chakula kutokana na maafa hayo huku wakiendelea kutafuta namna ya kutatua changamoto hiyo na wananchi wao kupata maeneo ya kuishi.