Prof. Muhongo apewa tuzo, kwa mchango wake kuleta maendeleo

By Sabato Kasika , Nipashe
Published at 12:25 PM May 16 2024
Mbunge wa Musoma Vijijini Profesa Sospter Muhongo.
Picha: Nipashe Digital
Mbunge wa Musoma Vijijini Profesa Sospter Muhongo.

JUMUIYA ya Wazazi ya CCM Mkoa wa Mara, imempa tuzo ya heshima Mbunge wa Musoma Vijijini Profesa Sospter Muhongo kwa mchango wake wa kutekeleza miradi ya maendeleo jimboni mwake.

Mwenyekiti wa jumuiya hiyo Mkoa wa Mara, Julius Kambarage ndiye aliyotoa tuzo hiyo.Tuzo hiyo imetolewa katika kilele Cha maadhimisho ya Wiki ya Wazazi katika Kijiji cha Bwai Kwitururu Kata ya Kiriba Musoma Vijijini.

Amesema, mbunge huyo amefanya makubwa katika utekelezaji wa Ilani ya CCM ya mwaka 2020/2025, hivyo hawana budi kumpongeza kwa mchango wake.
"Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Mara imeona impe tuzo ya heshima  mbunge huyo kwa kutambua mchango wake mkubwa kwenye utekelezaji wa miradi iliyoainishwa ndani ya Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020-2025, ' amesema Kambarage.

Viongozi wa jumuiya hiyo wakiwa na tuzo ya heshima walimpa Prof. Muhongo.
Mbunge huyo amesema uahirikiano kati yake na wananchi pamoja na serikali umechangia kulifanya jmbo kupiga hatua kwenda mbele.

"Bila uahirikiano ni vigumu kufikia maendele,  hivyo ninashukuru kwa jinsi tunavyoshirikiana na pia ninashukuru kwa tuzo ya heshima ya kutambua mchango wangu," amesema Prof. Muhongo.

Tuzo ya heshima aliopewa Prof. Muhongo.