WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimen-ti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Simbachawene ameaigiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kufanya utafiti na kuishauri serikali ili kuondoa migogoro ya ardhi nchini kutokana na kuwasababishia wa-nanchi maumivu makubwa.
Simbachawene alitoa agizo hilo jana wakati akifungua mafunzo ya wachunguzi wasaid-izi na wachunguzi wakuu 420 wa TAKUKURU katika Shule ya Polisi Moshi (TPS).
Alisema utafiti unaonyesha migogoro ya ardhi inatengen-ezwa na baadhi ya watumi-shi wasio waadilifu hali inay-opelekea viongozi kuwekeza nguvu nyingi katika utatuzi wa migogoro badala ya kufikiria maendeleo.
“Sekta hii imeleta migogoro mikubwa sana, imesumbua familia inaitesa jamii, kila mkoa, kila wilaya, kila kata, kijiji pana mgogoro wa ardhi, inadumaza maendeleo, inaharibu malengo ya baadhi ya watu.Umempa kiwanja B, una-shangaa kiwanja hicho hicho amepewa C na F na wote wana hati hivi tunashindwaje kuwatafuta hao wote waliohusika na kufanya hayo, kokote walipo waje wajibu? TAKUKURU isaidieni serikali hatutaki kusikia tena migogoro hiyo,” alisema na kuongeza kuwa:
“Kwa sasa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ( Jerry Silaa) anapita huku na huko kuhakikisha anatatua, lakini anakutana na watu wamegushi nyaraka nyingi sana zinazopelekea migogoro.
Tuna mifumo, lakini unakuta kiwanja kimoja kina michoro miwili na hati mbili, hii haikubaliki. Shiriki-aneni na Jeshi la Polisi, Tume ya Maadili katika kuweka mkakati wa kutokomeza jambo hili.
”Simbachawene aliwata-ka kuongeza nguvu kwenye maeneo ya kutolea huduma ili kukabiliana na tatizo kubwa lililopo katika eneo hilo.
“Wapo wenzetu wengine kuse-ma ukweli wamegeuza maeneo hayo kuwa ni sehemu yao ya kupata kiinua mgongo na uta-jiri,” alisema.
Akizungumza kuhusu waajiriwa wapya, Simbachawene, alisema licha kupitia kwenye mchakato mbalimbali wa upati-kanaji wa ajira, bado kuna mti-hani wa mwisho wa kuwahakik-ishia uhalali huo.
“Mchakato ulikuwa ni mkubwa, waombaji walikuwa 20,000 waliotakiwa ni 420, kuingia kwenye kundi hilo sio jambo dogo, lakini kama nilivyosema safari bado ndefu, katika miezi mitano ya mafunzo ndipo mtakapojihakikishia uhakika wa ajira hii.
“Nyinyi ni wasomi wa taalu-ma mbalimbali na mna uwezo mkubwa , kumbukeni mnaokwenda kuwafanyia uchunguzi huo nao ni wasomi kama nyinyi mkipambana kutoa elimu na wao wanapambana kuharibu ila shabaha ya serikali ni kuhakikisha inajenga chombo cha wanataaluma ambacho kita-fanya utafiti, kitazuia kwa mbinu mbalimbali mtakazofundishwa,” alisema Simbachawene.
Alisema chombo hicho kinahitaji watumishi waadilifu na wazalendo, wenye nidhamu ya kutosha ili kuleta taswira ra-hisi na kuongeza kuwa kazi yao itakuwa kutoa taarifa kwa mamlaka ikiwa kuna eneo lolote linaonekana kuwa na dosari.
“TAKUKURU ijikite zaidi ka-tika kuzuia na sio kupambana, unapofikia kupambana unaku-wa tayari umechelewa, hivyo ongezeni viherehere mpaka mtu hela ikiingia leo aseme moyoni, bora nikajenge tu darasa, kituo cha afya vionekane ili niache kufuatwa fuatwa na TAKUKURU, msipofanya hivyo watu wanaan-za mipango mara anapoona fedha.”
Awali, Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Kamishna wa Polisi, Salimu Hamduni, alisema kwa kipindi cha miaka mitatu, seri-kali imeipatia taasisi hiyo kibali cha kuajiri watumishi 1,190 na watumishi wa kubadili kada 102 ambao walijiendeleza.
Alisema wanafunzi wa mafunzo ya uchunguzi (wajunguzi wakuu 310) waliwasili shuleni hapo Mei 31, mwaka huu na wa-natarajiwa kukaa chuoni hapo kwa ajili ya kuanza mafunzo ya miezi mitano.
“Mafunzo yanatarajiwa kufanyika kwa nadharia na vitendo. Wiki tisa watafanya kwa vitendo, kila mwajiriwa wa TAKUKURU atapaswa atambue ya ajira yake itategemea uadilifu na nidhamu kwa muda wote wa maisha wake,” alisema.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu, alisema TAKUKURU ni jicho litakalochangia maendeleo na kuwataka wataalamu kutumia fursa ili kuongeza tija kwa taifa.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED