Simbachawene apongeza mageuzi ya kiteknolojia PSSSF

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 02:57 PM Jun 20 2024

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora, George Simbachawene (kushoto), akiangalia kwa karibu jinsi huduma za PSSSF zinavyopatikana kupitia mtandao, alipotembelea banda la Mfuko huo kwenye Maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma.
Picha: Mpigapicha Wetu
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora, George Simbachawene (kushoto), akiangalia kwa karibu jinsi huduma za PSSSF zinavyopatikana kupitia mtandao, alipotembelea banda la Mfuko huo kwenye Maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma.

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi, George Simbachawene, ameusifu Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) kwa kwenda sambamba na mabadiliko ya teknolojia katika utoaji huduma, kwani inasaidia uwazi na uwajibikaji.

Simbachawene ameyasema hayo jana baada ya kupatiwa maelezo na kuona jinsi Mfuko unavyotoa huduma kupitia mifumo ya kidijitali alipotembela banda la PSSSF kwenye Maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayofanyika Viwanja vya Chinangali jijini Dodoma.

Akitoa maelezo ya utoaji huduma kupitia mtandao (Online System), Afisa Mwandamizi wa Matekelezo PSSSF, Magira Werema alisema, muelekeo wa Mfuko ni kuachana na matumizi ya karatasi kwenye utoaji huduma na badala yake umejikita katiamkutoa elimu ya jinsi ya kutumia huduma kupitia mtandao.

1
Alisema hivi sasa Mwanachama anapokaribia kustaafu, anawzea kutuma madai (Claim notification), kupitia mtandao, hatua ambayo imeongeza uwazi katika utoaji huduma.

“Mfuko unaachana na utaratibu wa kujaza fomu nakala ngumu 'hard copy' badala yake madai yote yanawasilishwa kupitia Mtandaoni yaani PSSSF MEMBER PORTAL.” Alifafanua Bw. Werema na kuongeza.. Hivyo ni vema wanachama wa Mfuko wanaombwa kujisajili kwenye PSSSF MEMBER PORTAL ili kuwawezesha kupata taarifa zinazowahusu kwa wakati na uwasilishaji wa madai kuwa ni wenye ufanisi na uwazi, pia waajiri kuweza kulipia michango na kupata risiti kwa kujihudumia wenyewe.” alifafanua.
2

Aidha, kupitia huduma za PSSSF Kiganjani, mwanachama anaweza kupata huduma zote zinazohusiana na uanachama wake, ikiwa ni pamoja na kupata taarifa za michango yake, wastaafu nao wanaweza kujihakiki lakini pia kuuliza maswali na kupatiwa majibu.
3