THRDC kushiriki Kampeni ya Mama Samia Legal Aid Njombe

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 05:09 PM May 28 2024
Banda la Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC).
Picha: Mpigapicha Wetu
Banda la Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC).

MTANDAO wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) unashiriki kutoa elimu ya msaada wa kisheria katika uzinduzi wa Kampeni ya Mama Samia (Mama Samia Legal Aid Campaign) iliyozinduliwa mkoani Njombe.

Mkurugenzì wa THRDC Onesmo Ole Ngurumo ameviambia vyombo vya habari kuwa watatumia wiki hiyo mkoani humo kwa kuwafikia wananchi moja kwa moja kwa kutoa elimu za kisheria.

Amesema tayari wameshafikia wananchi wengi katika kutoa elimu ya sheria na haki za binadamu wenye uhitaji. "Tunafanya hii ikiwa ni juhudi za kuunga mkono Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kila mwananchi anastahili kupata elimu juu ya sheria" amefafanua

Waziri wa Katiba na Sheria Dk. Balozi Pindi Chana ametoa wito kwa wanasheria nchini kuisaidia Serikali katika utoaji wa elimu na kuisaidia jamii katika masuala ya haki za kisheria nchini. 

Nae Waziri wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia na Makundi Maalum, Doroth Gwajima amewapongeza wadau wote wanaoshiriki katika kampeni hizo na kusema kwamba wameisaidia Serikali kwa kiwango kikubwa kutatua migogoro mingi katika jamii.

"Nasisitiza tuendelee kuwasaidia Watanzania hasa walioko vijijini ili waweze kupata haki zao". Pia ametoa wito kwa Watanzania juu ya kupendana na kuheshimu haki za binadamu.