THRDC yawajengea uwezo watoto elimu ya Haki za Binadamu

By Pilly Kigome , Nipashe
Published at 11:04 PM Jun 19 2024
Mwenyekiti Jukwaa Haki Za Watoto Tanzania(TCRF) Sylvia Ruambo.
Picha: Pily Kigome
Mwenyekiti Jukwaa Haki Za Watoto Tanzania(TCRF) Sylvia Ruambo.

MTANDAO Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania(THRDC) wamekuja na mkakati wa kuwajengea uwezo watoto katika kuwapa elimu za utetezi wa haki za binadamu kwa kuanzisha na kuzindua majukwaa yatakayoendeshwa na watoto.

Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi THRDC Wakili Onesmo Olengurumo amesema wameona wajikite kuwapa uwezo watoto katika kuwapa elimu zihusuzo utetezi wa haki za binadamu ili waweze kujilinda wenyewe katika kukabiliana na baadhi ya majanga na kutambua haki zao za msingi.

Amesemá mfumo wa elímu uliopo sasa unachangamoto hauwajengi watoto kwa kiasi kikubwa katika kuwajenga katika kukabiana na kujitetea kwa kutambua haki zao.

"Tunataka watoto tuanze kuwajenga kuanzia chini katika msingi na wanapokuwa wanakua wawe wanatambua haki zao kwa kuwakutanisha katika majukwaa mbalimbali kuwajengea uwezo ikiwemo kukabiliana na soko la ajira la duni" amesema

Eunice Ishenda(11) mwanafunzi darasa la sita katika Shule ya Msingi Jerusalem.
Eunice Ishenda(11) mwanafunzi darasa la sita katika Shule ya Msingi Jerusalem ambae ni mgeni rasmi katika uzinduzi wa jukwaa hĂ­lo amesema anaiomba Serikali waangalie mazingira ya elimu hasa kwa watoto vijijini.

Pia aliomba kutungwa kwa sera za elimu ipasavyo ili watoto kufikia maono yao kwani watoto ni jeshi kubwa katika Taifa.
Wanafunzi wakifuatilia mafunzo hayo.

Ikiwemo kuomba kulindwa kwa watoto katiÄ·a majanga yanayowakuta ikiwemo ubakaji, ulawiti na ukatili mwingine utakaofanya watoto kukosa uhuru katika maisha ya kilasiku.

Kwa upande wake Mwenyekiti Jukwaa Haki Za Watoto Tanzania(TCRF) Sylvia Ruambo amesema jukumu la kuwalinda watoto ni la watanzania wote si la mtu mmoja na hatua hii iliyochukuliwa na THRDC ya kuwajengea uwezo watoto utaleta matokeo chanya na kuwa naTaifa imara.
Wanafunzi wakiwa katika picha ya pamoja.