Waziri wa fedha awasilisha makadirio ya mapato na matumizi 2024/25

By Frank Monyo , Nipashe
Published at 09:11 AM Jun 14 2024
Waziri wa Fedha, Dk. Mwingulu Nchemba.
Picha: Mpigapicha Wetu
Waziri wa Fedha, Dk. Mwingulu Nchemba.

Waziri wa Fedha, Dk. Mwingulu Nchemba leo amewasilisha bungeni Mapendekezo ya serikali kuhusu makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka 2024/25.

"Napenda kutumia fursa hii kumpongeza sana Mheshimiwa Dk. Samia Suluhu Hassan, kwa uongozi wake shupavu ambao umedhihirishwa wazi na majira ambayo nchi imepitia. Ikumbukwe kuwa, Mheshimiwa Rais alipokea usukani wa kuiongoza nchi ikiwa imepatwa na tukio la huzuni la kuondokewa na aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Dk. John Magufuli, tukio ambalo halikuwahi kutokea hapa nchini lakini MAMA hakuyumba na hata sasa tunasonga mbele, nchi haijakwama kwenye jambo lolote,Nchi inasonga mbele!"- Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba