Wenye simu za 'kitochi' kukata tiketi kidigitali treni ya umeme

By Frank Monyo , Nipashe
Published at 01:04 PM May 28 2024
Mashine za kukata tiketi kwa ajili ya safari za treni ya umeme kidigitali.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli nchini (TRC), Masanja Kadogosa amesema kuwa baada ya kukamilika mfumo wa tiketi treni SGR, abiria ambaye atumii simu janja (smart phone) atakuwa na uwezo wa kukata tiketi yake kidigitali.