Wizara ya Mambo ya Ndani yaibuka mshindi wa pili kutoa taarifa kwa umma

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 07:09 PM Jun 18 2024
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni.
Picha: Maktaba
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni.

Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi imeibuka mshindi wa pili kati ya wizara 10 Bora kwa kutoa taarifa kwa umma kupitia vyombo mbalimbali vya habari katika kipindi cha mwaka 2023/2024.

Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Thobias Makoba ametangaza ushindi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi mbele ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan wakati wa Kongamano la Maendeleo ya Sekta ya Habari na Kikao Kazi cha Maafisa Habari wa Serikali kilichofunguliwa leo katika Ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam.


Kongamano hilo la pili la Maendeleo ya Sekta ya Habari nchini lililofunguliwa na Rais Samia limehudhuriwa na wadau mbalimbali wa habari, mabalozi na Miongoni mwa Makatibu Wakuu waliohudhuria ni Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Ally S. Gugu na Viongozi wengine wa Serikali.