AKITANGAZA BAJETI YA NNE... Sura kuu nne za Samia kutekeleza maendeleo

By Peter Orwa , Nipashe
Published at 04:24 PM Jun 21 2024
Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, akipokea ripoti ya Kamati Maalum ya Corona, aliyoiunda, mwaka 2021.
PICHA: MTANDAO
Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, akipokea ripoti ya Kamati Maalum ya Corona, aliyoiunda, mwaka 2021.

HADI sasa Serikali ya Awamu ya Sita ina hesabu ya miaka mitatu na ushee. Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, jana ikiwa mara ya nne ilisomwa bajeti ya serikali chini ya uongozi wake.

Wengi wamekuwa wakimfuatilia mwenendo wa zama zake za kiutendaji wana sura tofauti. Lakini katika mantiki ya saikolojia ya mwenendo wa uendeshaji uchumi wa nchi katika Awamu ya Sita ya Uongozi wa Maendeleo nchini, inaweza kugawanyika katika makundi makuu manne. 

Mosi, ambako ndiko kwenye mzizi wake ni ilani, pia sera za chama chake CCM, uongozi uliopo ukielekezwa kutekeleza ndani ya kipindi maalum, ikwamo misimu ya uongozi. 

Pili, ndani yake ni dira za kihistoria katika mipango ya maendeleo nchini, ambayo kwa kina inazama katika ubunifu uliofanywa baada ya uhuru; Mpango wa Kwanza wa Miaka Mitano wa Maendeleo ya Tanzania 1964-1969, ikiambatana na yaliyoamuliwa makuu kitaifa, kuambatana nayo kwa wastani wa miaka minne mfululizo, hata ikadumu baada ya hapo. 

Imani na dira ya kimaendeleo ya kudumu, ndio inayowawezesha Watanzania kufanikiwa kisekta katika maeneo kama elimu, kilimo na afya, imekuwa itikadi ya kudumu na ina historia tangu mwaka  1964, kuwafanikisha na ndio maana hata sasa Rais Dk. Samia, naye anaendeleza kulingana na mahitaji ya kisasa. 

Mathalan, kwa sasa kuna wigo wa elimu bure, maboresho katika sekta ya afya kama bima ya afya, kuwawezesha wazee na kinamama katika nafasi hiyo, huku kukiwapo mapinduzi ya viwango vya huduma, kuanzia mindombinu, vifaa na utaalamu. 

Hicho ndicho kinaonekana katika uwekezaji mkubwa katika sekta ya kilimo, bajeti yake ikikuzwa maradufu, kuleta mapinduz ya soko na teknolijia, kama ilivyo katika elimu, kubeba mfano Awamu ya Kwanza bajeti kufika asilimia 25. 

Eneo lingine analotafsiriwa Rais Dk. Samia, inafafanuliwa katika mipango ya uongozi wake, una sura ya kuendeleza mazuri ya kimaendeleo yaliyojitokeza zaidi katika mfumo huria wa uchumi, hasa yaliyojiri Awamu ya Pili na Tatu ya uongozi wa nchi, ikikumbukwa Rais Benjamin Mkapa, akitamka ‘serikali itabaki mratibu mkuu wa shuguli na biashara kubakia katika sekta binafsi.’ 

Lakini, penye sura ya tatu anaporejewa Rais Dk. Samia ni katika staili ya uongozi na mipango yake ya maendeleo, daima hajaachana kitaaluma na alichukulia darasani; Utawala wa Umma, Uchumi na Maendeleo ya Kiuchumi.

Lakini, kama ilivyo msimamo wa viongozi wote wakuu wa nchi katika Awamu Tano zilizotangulia katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano, daima hazijawahi kuwa mbali na mtazamo mkuu wa misingi iliyoundwa na serikali ya Awamu ya Kwanza. 

Hiyo imebaki kuwa dodosi kuu la sasa na awamu zote zilizotangulia, zimekuwa katika sura ya pamoja kutekeleza msingi wa Awamu ya Kwanza, kupitia Mpango wa Maendeleo wa Kwanza wa Mwaka 1964 na yaliyojitokeza baada ya hapo, mathalani miradi mikubwa ya kitaifa, Reli ya SGR ambayo ina mzizi kuanzia zama za Awamu ya Tatu, pia mradi mkubawa umeme kutoka Awamu ya Kwanza

·          Kuanzia Ijumaa ijayo, fuatilia safari ya maendeleo ya nchi tangu uhuru wa nchi, mwaka 1964.