Benki yawekeza ‘CSR’ Kanda Ziwa ikifuta vifo vya mama, mtoto wodini

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 06:47 AM Apr 18 2024
•	Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya Mwanangwa, wilayani Misungwi mkoa wa Mwanza, Consolata Simba, akionyesha baadhi ya vitanda, magodoro na mashuka walivyopokea.
Picha: Maktaba
• Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya Mwanangwa, wilayani Misungwi mkoa wa Mwanza, Consolata Simba, akionyesha baadhi ya vitanda, magodoro na mashuka walivyopokea.

KITAIFA inaelezwa mafanikio yanayoendelea, imo kupungua vifo vya mama na mtoto. Ni matokeo ya kuimarika huduma za afya nchini, pia uwekezaji kiserikali na mchango wa wadau.

Hapo kuna sekta za umma na binafsi na Kanda ya Ziwa, sasa inatajwa kuwa sehemu ya mnufaika mkubwa wa vifaa tiba, inayotolewa na benki hiyo kuzisaidia hospitali na vituo vya afya. 

Msingi wake azma ya serikali ni kuboresha ubora na kurahisisha upatikanaji wa matibabu na huduma nyingine mtambuka.

 Kwa mujibu wa Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Buzuruga mkoani Mwanza, Dk. William Mtinginya, ufadhili umesaidia kupunguza kwa kiasi kikubwa vifo na maradhi, bali pia umesaidia kuongeza idadi ya akina mama na watoto wachanga wanaohudumiwa.

 “Tumeweza kupunguza idadi ya vifo vinavyoweza kuzuilika vya wazazi na vichanga lakini pia wateja wa huduma ya uzazi wameongezeka na sasa wazazi wapya 20 wanahudumiwa hapa kwetu kila mwezi,” Dk. Mtinginya anatamka wilayani Ilemela.

 Takwimu zinaonyesha wastani theluthi moja ya vifo vyote vya watoto nchini vinatokana na watoto sababu zinazoweza kuzuilika, pia magonjwa  yanayotibika pamoja na uhaba wa vifaa vya kuwahudumia.

 Wataalamu wa afya wanafafanua kuwa vifo vingi vya hutokana na changamoto za afya za kinamama wanapokuwa wajawazito na mazingira duni ya kujifungulia.

Hapo ndio wadau, benki ya NMB imeangaza shida hiyo na kuamua kuchangia, kuziba pengo la mapungufi katika afya kusaidia hali hiyo,

 Kwa sasa, ufadhili wake umesaidia sana kulidhibiti kwa kiasi kikubwa tatizo hilo la kiafya katika Kanda ya Ziwa inayojumuisha mikoa minne, sasa viongozi, wanufaika Kanda ya Ziwa wanakiri imechangia kwa kiasi kikubwa kuboresha huduma za uzazi, mama na mtoto katika mikoa ya kanda hiyo; Mara, Kagera, Mwanza na Geita. 

KUTOKA NMB 

Wawakilishi wa NMB makao makuu, wanasema vitanda vya kawaida na vya kujifungulia wazazi, magodoro na vifaa tiba vingine wanavyovitoa, vimekuwa ni uwekezaji wenye tija na afua muhimu katika kusaidia kuokoa maisha ya akina mama wajawazito na watoto.

 Kwa mujibu wa sheria ya nchi, taasisi zote zina wajibu kurejesha faida kwa jamii, kupitia kinachoitwa kitaalamu kama ‘corporate social responsibility.’

 Ujumbe wa NMB ulikuwa katika ziara ya kutathimini shughuli za uwajibikaji wake kwa jamii katika mikoa mitatu ya kanda hiyo, ukifahamishwa uhalisia wa thamani hiyo inavyowaafikia wananchi; kuwaboreshea wana -afya mazingira ya kuwahudumia wazazi na watoto.

 "Sambamba na dhamira yetu ya kurudisha fadhila kwa jamii, tunawekeza vya kutosha katika programu mbalimbali endelevu za kijamii kwa kila mwaka kutenga asilimia moja ya faida baada ya kodi katika shughuli za CSR," Meneja wa NMB Kanda ya Ziwa, Wogofya Mfalamagoha.

“Mwaka jana, bajeti hii ilifikia zaidi ya shilingi bilioni sita, pia kukidhi shughuli za uendelevu ambazo zilijumuisha upandaji miti kote nchini kwa ajili ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi,” anasema Wogofya.

 TIMU YA MATABIBU

 Mikoa iliyotembelewa ni Geita, Mara na Mwanza, huku Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Buzuruga mkoani Mwanza, Dk.William Mtinginya, akifafanua alivyonufaika na misaada hiyo: 

 “Tumeweza kupunguza idadi ya vifo vinavyoweza kuzuilika vya wazazi na vichanga, pia wateja wa huduma ya uzazi wameongezeka na sasa wazazi wapya 20 wanahudumiwa hapa kwetu kila mwezi.”

 Dk. Mtinginya anaiambia timu hiyo iliyomtembelea kituoni hapo wilayani Ilemela, kwamba: “Kabla ya ufadhili wa vifaa kutoka NMB tulikuwa tunawahudumia wajawazito 200 hadi 300 kwa mwezi. Lakini, sasa hivi wamefika 600, huku idadi ya wanaojifungulia majumbani nayo ikipungua sana.”

 Katika Kituo cha Afya Katoro mkoani Geita, Dk Rhoda Haule anaomba usaidizi zaidi kutoka taasisi nyingine za sekta binafsi, akisisitiza umuhimu na uhitaji wake katika kuyanusuru maisha ya wazazi na watoto wachanga.

 Mganga huyo anataja moja ya faida za vitanda vipya ni kuondokana na changamoto ya kina mama kulala watatu hadi watano kwenye kitanda kimoja, wakisubiri kujifungua.

 Anasema, pamoja na kuboreka huduma kwenye wodi za wazazi ambazo sasa zinawahudumia wajawazito kati ya 750 hadi 900 kila mwezi, bado kuna umuhimu wa kufanya maboresho zaidi.

 “Jumla tuna vitanda 102, kwahiyo huduma zetu zitaimarika zaidi endapo tutapata wafadhili wengine,” anaeleza

 Benki hiyo, pia inapongezwa kwa msaada wa vitanda, mashuka na magodoro iliyopata zahanati ya Mwanangwa inayohudumia wakazi 20,000 wa Kata ya Mabuki na vijiji vya jirani wilayani Misungwi, Mwanza.

 Dk. Consolata Simba, anasema huduma ya afya ya Mama nA Mtoto, ni suala mtambuka katika kuokoa maisha, kuimarisha ustawi wa jamii na kuchochea maendeleo ya taifa kwa ujumla.

 Mganga huyo anasema, baadhi ya vifo vya mama na mtoto hutokana na umbali wa kufikia huduma stahiki, pamoja na kinamama kujifungua kienyeji majumbani.

 Pia, anataja upungufu wa wahudumu wa afya wenye ujuzi wa kutosha, ukosefu wa vifaa tiba vya msingi, kutokuwepo kwa mfumo unaojitosheleza wa rufaa pamoja na huduma duni za dharura za uzazi na watoto wachanga.

 Wataalamu wa afya za watoto wanasema vingi vya vifo hivi Hutokana na changamoto za afya za akina mama wanapokuwa wajawazito na mazingira duni ya kujifungulia na kuvilea vichango hali inayoonyesha unyeti wa mchango wa Benki ya NMB katika maendeleo ya sekta ya afya nchini.

 Wilayani Serengeti, Mganga Mfawidhi Dk. Juma Rajabu Ali, anasema kujengwa wodi ya kisasa, ambayo ikikamilika mwezi ujao, itawezesha wajawazito wanne kujifungua kwa wakati mmoja, ikilinganishwa na wawili au watatu wanaojifungua kwa siku sasa.

Aidha, Dk. Juma anataja kuna manufaa ya kupunguzwa vifo vya watoto wachanga kwa sasa ni asilimia 12 hadi15, anafafanua: “Kupatikana ufadhili huu kwa wakati kusaidia kuukamilisha mradi huu wa ujenzi kumewagusa viongozi na wananchi kwa sababu ya umuhimu wake katika maisha ya wananchi wa hapa,”