Chongolo aanza na ziara kukagua bilioni 32/- alizowekeza Samia, kuugeuza mkoa

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 01:51 PM May 24 2024
news
Picha: Yasmine Protace
Mkuu wa Mkoa, Daniel Chongolo, akikagua moja ya madaraja yanayojengwa mkoani kwake.

KATIKA mgawanyo wa pesa kitaifa, Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, Sh. bilioni 32 kuendeleza miradi ya mkoani Songwe, Mkuu wa Mkoa mpya, Daniel Chongolo, akijumuisha ziara yake ya kwanza, akiikagua.

Ni miradi mkoani hapo, inayaotekekezwa kwa miaka mitatu sasa, ikitumia fedha hizo, hiyo wiki iliyopita, ambako akazungumza na wakazi, ikiendana na kuwashauri na kuagiza, pale alipoona kasoro.

Ni ziara yenye ajenda kuu, kujenga umoja na mshikamano katika juhudi za maendeleo, kukemea maovu na ukatili wa kijinsia, mila potofu, ubakaji, ukatili wa kingono kwa watoto, mimba na ndoa za utotoni, ubadhilifu wa fedha za umma na lishe duni.

Siku ya kwanza alianza kukagua Shule ya Wasichana ya Ileje, akigawa jezi na mipira kwa wanafunzi. Hata hivyo, akanika kasoro ya rekodi mbaya ya kuwapo wenye ufaulu daraja sifuri 100, katika matokeo ya mitihani ya kidato cha nne.

Hapo, akawaelekeza walimu na maofisa elimu kuhakikisha wanainga katika mikakati ya shule ya ufaulu darasa sifuri, wanafunzi wote waangukie lengo la madaraja ya kwanza na pili.

KILIO KUCHELEWA MIRADI

Miradi mingine aliyotembelewa ni ya elimu, afya, maji, miundombinu ya barabara na madaraja, Mgodi wa Makaa ya Mawe wa Stamico na kituo cha forodha kilichopo mpakani mwa Malawi na Tanzania.

Baada ya hapo Chongolo aliyekwishakuwa mkuu wa wilaya mbili tofauti, kisha Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), mahali alikoanzia akiwa ofisa, akitokea kwenye uandishi vyombo vya habari, akawa na mkutano nja umma, akipokea kero zao.

Kero kubwa inayoonekana ni kuchelewa kwa ujenzi wa mradi wa maji wa Itumba -Isongole na jengo la utawala, huku akitoa maelekezo ya kuhakikishwa miradi hiyo inakamilika kwa wakati, ukiwamo wa barabara na daraja kwenye Mgodi wa Stamico, miradi mingine ikionekana iko vizuri.

Aidha, anawasifu wananchi wa Ileje kulima mazao mengi akikosoa kasoro yao ni kutojua kuipangilia mlo kamili, akisema hali ya udumavu kwa watoto chini ya miaka mtano sasa ipo juu, akiwasihi wale vyakula mchanganyiko, iwafae kiafya.

Pia, Chongolo akawageukia uso wanaume wa Songwe, dhidi ya kasi yai kuwapa mimba mabinti, hasa wa masomoni, akaliagiza jeshi la polisi, kuhakikisha linawakamata watakaobainika kusababisha ujauzito, hasa wanafunzi kwa ajili ya hatia za kisheria, huu akiwasihi wazazi kutowaozesha watoto chini ya umri huo.

“Rais Dk.Samia ameleta fedha nyingi zaidi ya bilioni 32 katika kipindi cha miaka mitatu ya urais wake. Fedha hizo zimejenga miradi mingi ikiwamo ya elimu, lengo watoto wasome ili wawe viongozi wa baadae na si kuwaharibia Maisha. Nitakayembaini ‘nitakula sahani moja’ naye,”anasema.

MAENDELEO YA AFYA

Mganga Mkuu wa Mkoa Songwe, Dk. Boniface Kasululu, anaifafanua Ripoti ya Utafiti wa Kidemografia Mwaka 2022, kwamba kiwango cha huduma kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano kimepungua, kutoka asilimia 43 hadi 31.9.

Analalamika kwamba, kiwango hicho bado ni kikubwa, ikilinganishwa na kiwango cha kitaifa asilimia 30 na kiwango cha unyonyeshaji maziwa ya mama mkoa una asilimia 60.7, wakati kitaifa ni asilimia 59 na kupitia takwimu hizo, wanaendelea kutoa elimu ya kuhakikisha viwango ama vinashuka au kumalizika kabisa.

Anasema, katika kudhibiti latizo la lishe duni mkoani Songwe, wanatekeleza afua mbalimbali za kukabiliana na tatizo la lishe, ikiwamo kusimamia utekelezaji wa mkataba wa viashiria vya lishe na mpango mkakati jumuishi, kupinguza udumavu kwa 2021/2022 hadi 2025/2026. 

Kutokana na hali hiyo mkuu huyo wa mkoa, anawataka wananchi kuunga mkono jitihada za serikali kuhakikisha mambo yote yana yokatazwa yanamalizika na kuufanya mkoa kuwa wa kihistoria kwa mambo mazuri na si mabaya.

     Mkuu wa Mkoa, Daniel Chongolo, akikagua moja ya madaraja yanayojengwa mkoani kwake. PICHA ZOTE: IBRAHIM YASSIN.