Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran yatoa taarifa kuhusu mashambulizi dhidi ya Israel

By Mwandishi Wetu , Nipashe Jumapili
Published at 04:01 PM Apr 14 2024
Waziri wa Mambo ya Nje ya Iran, Hossein Amirabdollahian.
Picha: Ubalozi wa Iran Tanzania.
Waziri wa Mambo ya Nje ya Iran, Hossein Amirabdollahian.

Waziri wa Mambo ya Nje ya Iran, Hossein Amirabdollahian, katika taarifa yake kufuatia mashambulizi ya kijeshi kwenye vituo vya kijeshi vya Israel yaliofanywa na Majeshi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran leo Aprili 14,2024 ameeleza kuwa huko ni kujibu na kutumia haki yake ya kujilinda kama ilivyoainishwa katika Ibara ya 51 ya Mkataba, dhidi ya mashambulizi ya kijeshi ya mara kwa mara ya Israeli, yaliyosababisha kuuawa kwa washauri wa kijeshi wa Iran waliopo Syria kwa mwaliko wa serikali ya Syria, hasa shambulio la Aprili 01,2024 katika majengo ya kidiplomasia ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran huko Damascus.

Waziri huyo amesema kuwa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inathibitisha tena azma yake kwa madhumuni na kanuni za Mkataba wa Umoja wa Mataifa na sheria ya kimataifa, wakati ikisisitiza azma yake ya kulinda kwa nguvu uhuru wake, uadilifu wa ardhi yake na maslahi ya kitaifa dhidi ya matumizi yoyote haramu ya nguvu na mashambulizi.

Amesema matumizi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ya hatua za kujilinda kama sehemu ya haki yake ya kujilinda yanadhihirisha mbinu ya kuwajibika ya Iran kuelekea amani na usalama wa kikanda na kimataifa wakati utawala wa kibaguzi wa ukaliaji unaoendelea na kampeini ya mauaji dhidi ya watu wa Palestina unakwenda sambamba na mashambulizi ya kijeshi mara kwa mara dhidi ya Mataifa jirani na kuchochea moto katika eneo na zaidi.

Ameongeza kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran haitasita kuchukua hatua za kujilinda zaidi kuhifadhi maslahi yake halali dhidi ya vitendo vyovyote vya uchokozi wa kijeshi au matumizi yoyote haramu ya nguvu.