Dk.Nchimbi awaahidi barabara ya lami Mlele, "Nitamwambia Rais Samia"

By Halfani Chusi , Nipashe Jumapili
Published at 07:01 PM Apr 14 2024
news
Picha: Halfan Chusi
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk.Emmanuel Nchimbi akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Makongoro Nyerere alipofika mkoani kwaajili ya kuendeleza ziara yake.

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk.Emmanuel Nchimbi amewaahidi wananchi mkoani Katavi kufikisha kilio cha kutaka kujengewa barabara kwa kiwango cha lami kwa Rais Samia Suluhu Hassan ili waondokane na adha ya usafiri.

Pia amewaahidi kwamba CCM kwa kushirikiana na serikali wataendelea  kuwashika mkono wakulima kwa kupumguza bei ya mbolea na kurahisisha upatikanaji wake.

Kiongozi huyo ameyasema hayo leo, aliposimama kuwasalimia wakazi wa eneo la  kibaoni Wilaya ya Mlele wakati alipokuwa akielekea Mkoa wa Rukwa  kwaajili mwendelezo wa ziara yake.

"Nitamwambia Rais, ujenzi wa barabara hii uende kwa kasi ya mbwa koko kwa kasi ya haraka, mimi mwenyewe nimepita nimejionea hali ilivyo" amesema Nchimbi huku akishangiliwa na wafuasi wa chama hicho waliokuwa wamefurika kupokea salamu zake.

Akiwa Rukwa Katika mkutano wa hadhara uliofanyika  Katika Wilaya ya Nkasi mkoani humo amewahakikishia wananchi hao kutatua kero ya Maji na Kituo Cha afya liyolalamikiwa na baadhi ya wananchi.

Amesema amearifiwa kuwa eneo hilo lina tatizo la maji  na kwamba taarifa alizonazo tayar Waziri wa Maji Jumaa Aweso alitoa Sh milioni 300 kati ya 700 zilizokuwa zinahitajika.

"Sasa kuhusu hiyo Milioni 400 iliyobaki, ngoja nimpigie mwenyewe Waziri wa maji aseme hapa mumsikie" alisema 

Alipompigia Waziri Maji Juma Aweso amesema "Kesho jumatatu nitamuagiza katibu mkuu hizo fedha zilizobaki zitoke zije kukamilisha huo mradi, maelekezo ya chama kwetu sisi ni utekelezaji, lakini tutahakikisha dhamira ya Rais na ilani ya chama inatekelezwa" alisema aweso kwa njia ya simu mbele ya wananchi alipopigiwa simu na Nchimbi

Kuhusu kituo cha afya  alisema ameuagiza uongozi wa wilaya hiyo kushughulikia tatizo hilo mapema iwezekanavyo.

Amesema CCM imejidhatiti kuwasaidia watanzanja akisistiza mkoa huo ni moja ya mikoa inayozalisha chakula kwa wingi na kuliingizia pato taifa.

Katika mkutano huo Katibu wa NEC Itikadi Uenezi na Mafunzo CCM Amos Makalla, alisikiliza kero 15 kati yake 12 zilitafutiwa ufumbuzi na 2 zilichukuliwa kwaajili ya uamuzi kutoka ngazi ya juu. 

"Tunaitumia njia ya kisayansi kusikiliza kero kimya kimya wengine wanamalalmiko ya faragha siyo busara kumruhusu kila mtu aongee kwa sauti hapa hiyo siyo busara" alisema Makalla 

Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) Taifa Organaizesheni, Issa Gavu aliwataka wanachi hao kuchagua viongozi wa CCM Katika uchaguzi ujao kwa kile alichodai wameonja joto la jiwe kumchagua wa upinzani.

 "Mmejifunza na ninadhani hamto rudia tena kosa hilo, ninaomba msifanye tena kosa, sisi tunawahakikishia yale yote tutakayoahidi tutayatekeleza CCM imedhamuria kubomoa kata na majimbo yaliyopotea.

"Mtumie salama kwa Mbunge wa CHADEMA kwamba muda wake umekwisha, mtume salamu tena na sisi tunachotaka viongozi wetu wa wilaya na mkoa hakikisheni wagonbea mtakao wasimamisha wanakuwa na sifa na nguvu ya ushawishi" amesema Gavu