Majaliwa mgeni rasmi Baraza Eid el Haj kesho

By Romana Mallya , Nipashe Jumapili
Published at 08:34 AM Jun 16 2024

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.
Picha: Maktaba
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa, kesho anatarajia kuwa mgeni rasmi kwenye Baraza la Eid kitaifa litakalofanyika katika msikiti wa Mfalme Mohamed V1, Baraza Kuu la Waislam Tanzania (BAKWATA), Kinondoni, Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa taarifa ya Katibu Mkuu BAKWATA, Alhaj Nuru Mruma, wameomba waislamu kujumuika kwa wingi kushiriki swala hiyo.

“Tunaomba Wasilam kujumika kwa wingi kushiriki swala na Baraza la Eid kuanzia saa 1:00 asubuhi,” alisema.

Mruma alisema kwa niaba ya BAKWATA, Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Dk. Abubakar Zubeir anawatakia waislam na wananchi wote maandalizi mema ya sikukuu hiyo.