"Msiwasahau watoto wa kiume katika malezi yenu"

By Rashid Nchimbi , Nipashe Jumapili
Published at 03:49 PM May 26 2024
Mkuu wa Dawati la Jinsia na watoto Wilaya ya Monduli mkoani Arusha Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Jacqueline Uhwelo,
Picha: Polisi Monduli
Mkuu wa Dawati la Jinsia na watoto Wilaya ya Monduli mkoani Arusha Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Jacqueline Uhwelo,

Mkuu wa Dawati la Jinsia na watoto Wilaya ya Monduli mkoani Arusha Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Jacqueline Uhwelo, amewakumbusha wazazi kuwa, elimu wanayoitoa kwa watoto wa kike dhidi ya vitendo vya ukatili pia ugeukie kwa watoto wa kiume.

Wito huo umetolewa, kwenye kikao cha wazazi wa wanafunzi kilichofanyika katika shule ya Sekondari Olkeswa iliyopo wilayani Monduli.

Mkuu huyo wa Dawati alisema kumekuwa na kasumba kwa baadhi ya wazazi kuona kwamba, watoto wa kike wapo kwenye hatari zaidi dhidi ya vitendo vya ukatili huku wakilisahau kundi la watoto wa kiume.

Alisema kwa dunia ya sasa makundi yote ya watoto hayapo salama hivyo wazazi wanapaswa kuchukua hatua kwa kuwaelimisha lakini pia kuwafuatilia kwa ukaribu.

"Wazazi, tengeni muda wa kuzungumza na watoto wenu bila ubaguzi ili muweze kubaini changamoto wanazokumbana nazo". Alishauri mkuu huyo wa Dawati la Jinsia na watoto.