Rais Samia ateua tena

By Romana Mallya , Nipashe Jumapili
Published at 04:19 PM Apr 14 2024
RAIS Samia Suluhu Hassan.
PICHA: IKULU
RAIS Samia Suluhu Hassan.

RAIS Samia Suluhu Hassan amemteua Balozi Said Othman Yakub kuwa Balozi wa Tanzania nchini Comoro.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Zuhura Yunus, Balozi Yakub anachukua nafasi ya Balozi Pereira Silima ambaye amemaliza muda wake.

Pia juzi, Rais Samia alimteua CPA Anthony Kasore kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA).

“Kabla ya uteuzi huu, CPA Kasore alikuwa akikaimu nafasi hiyo,’ ilisema taarifa hiyo.

Rais pia alimteua Goodluck Shirima kuwa Kamishna wa Petroli na Gesi, Wizara ya Nishati.  Shirima kabla ya uteuzi huo, alikuwa Mkuu wa Kitengo cha Sheria na Uhusiano wa Kampuni ya Mafuta ya Puma Energy Tanzania.

Rais Samia tangu aingie madarakani miaka mitatu iliyopita, amekuwa akifanya uteuzi na utenguzi mara kwa mara ikiwa ni sehemu ya kuimarisha serikali ili kuendana na kasi anayoitaka.