Sunday adaiwa kubaka kuku hadi kufa

By Mwandishi Wetu , Nipashe Jumapili
Published at 12:52 PM Apr 14 2024
Adaiwa kubaka kuku hadi kufa.
PICHA: MAKTABA
Adaiwa kubaka kuku hadi kufa.

KIJANA mmoja aliyefahamika kwa jina la Sunday, mkazi wa Kitongoji cha Misungwi Kata ya Usagara wilayani Misungwi mkoani Mwanza, anadaiwa kubaka kuku hadi kufa.

Baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo wamesema mtuhumiwa alimkamata kuku huyo ambaye alikuwa anataga kisha kumuingiza ndani ya nyumba yake na kuanza kumbaka na baada ya kumaliza haja zake akatoka kumtupa nje. 

Mmoja wa wapangaji katika nyumba hiyo, Delifina Boazi amesema alitoka nje kwenda kukinga maji bombani ndipo alipomuona mtuhumiwa akifanya kitendo hicho sebleni akiwa amekaa kwenye makochi.

"Nilimuoma alikuwa amemkamata kuku na anafanya naye mapenzi na alipomaliza alienda kumtupa," amesema Delifina

Akizungumzia tukio hilo, Mwenyekiti wa kitongoji cha Misungwi, Samson Madirisha amekiri kupokea taarifa hizo na baada ya kufika eneo la tukio alikuta kitendo hicho kimeshafanyika. 

Madirisha amesema baada ya mtuhumiwa kuhojiwa alikiri kufanya kitendo hicho na kueleza kuwa alikuwa na hamu hivyo alishindwa kujizuia.

Naye Kamanda wa Sungusungu kata ya Usagara, Buhili Makubilo na mkazi wa eneo hilo Edista Mganga wameviomba vyombo vya dola kuwachukulia hatua watu wanaobainika kufanya vitendo hivyo. 

Hata hivyo, mtuhumiwa amechukuliwa na Jeshi la Polisi kwa ajili ya mahojiano zaidi.