Watetezi walia utumikishwaji wa watoto, waomba mabadiliko ya sheria na sera

By Pilly Kigome , Nipashe Jumapili
Published at 10:04 AM Jun 09 2024
Watetezi Walia Na Utumikishwaji Wa Watoto Waomba Mabadiliko Ya Sheria Na Sera.
Picha: Pilly Kigome
Watetezi Walia Na Utumikishwaji Wa Watoto Waomba Mabadiliko Ya Sheria Na Sera.

KUELEKEA June 12 siku ya Kimataifa ya kupinga utumikishwa kwa watoto Mtandao wa Watetezi Haki za Binadamu (THRDC) waiomba Serikali kubadilishwa kwa baadhi ya sheria, sera,kanuni na vipengele katika haki za watoto.

Akizungumza jijini Dar es Salaam Mratibu Kitaifa wa Mtandao wa Kupinga Utumishwaji kutoka THRDC,  Scolastica Pembe amesema muda umefika wa kuiomba Serikali kurekebisha baadhi ya vipengele katika hivyo ili kumlinda mtoto katika baadhi ya sheria kandamizi.

Amesema wameandaa kongamano hilo kwa lengo la kuwakutanisha wadau mbalimbali wa haki za binadamu ili kuangalia upya sheria za kumlinda mtoto hasa katika suala la malezi, ukatili na utumikishwaji wa watoto.

Amefafanua katika Sheria ya ndoa inaruhusu mtoto kuolewa chini ya umri wa miaka 18 lakini pia sheria ya kazi inaruhusu mtoto kufanya kazi katika umri huo,  lakini katika sheria hizo zinamtaka mtoto huyo apate muda wa kupumnzika na asifanye kazi hatarishi kwa hiyo kuna umuhimu mkubwa wa kubadilisha sheria hizo na vipengele katika kumlinda mtoto.

“Kwanza kabisa sheria hizo zinakinzana na sheria za haki watoto kwani mtoto ni yule aliye chini ya miaka 18, na inawezekana vipi mtoto huyo amekabidhiwa majukumu makubwa kama nyumba na mume na anatapata wapi muda wa kucheza hivyo kuna umuhimu wa kuangalia upya sera na sheria” amesema

Naye Mwenyekiti Kamati ya Maandalizi Kongamano hilo, Ibrahimu Samata amesema sababu kubwa ya utumikishwaji wa watoto mijini na vijijini ni umasikini uliokithiri.

Hivyo ameiomba na  kuihimiza serikali kuendeleza kutekeleza mipango madhubutu kuimarisha uwezo wa kaya mipango ya maendeleo katika  kupunguza umasikini.

Ikiwemo na kuunda kuangalia  sheria, sera kanuni miongozo katika kanuni za kumlinda mtoto ambapo takwimu zinaonyesha kuna watoto  Milioni nne (4) hadi tano(5) wanatumikishwa katika sekta ya kilimo hasa katika mikoa inayozalisha vyakula kwa wingi ikiwemo Simiyu, Kahama.

“Tunaamini kukipatikana kwa mabadiliko ya sheria na kupatikana kwa mikakati ya kuondoa umasikini tutaondokana na janga hili la utumikishwaji wa watoto nchini” amefafanua