Kampuni ya Sanku, yapongezwa kujikita kurutubishaji wa vyakula nchini

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 09:30 AM May 26 2024
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge na Uratibu) Jenista Mhagama akizungumza na watendaji mbalimbali aliopotembelea Kiwanda cha Sanku kilichopo Mwenge Jijini Dar es Salaam.
Picha: Mpigapicha Wetu
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge na Uratibu) Jenista Mhagama akizungumza na watendaji mbalimbali aliopotembelea Kiwanda cha Sanku kilichopo Mwenge Jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge na Uratibu) Jenista Mhagama amesema mahitaji ya virutubishi vya chakula ni ajenda kubwa ambayo itachochea katika kuongeza ajira kwa wakulima wetu na kuwa na uhakika na virutubishi tunavyovitumia hapa nchini.

Waziri amesema hayo alipotemebelea na kukagua kiwanda cha Sanku kilichopo Mwenge Jijini Dar es salaam Jana na kujionea maendeleo ya kiwanda hicho cha uchanganyaji wa virutubishi kwenye unga wa mahindi na ngano kwa bei nafuu.

Naomba muendeele kufanya ufutailiaji wa karibu katika kutoa elimu ili kuondoa matatizo mengine ya udumavu, utapiamlo na shida ya kupungukiwa vitamini A kwa wakinamama wajawazito.

“Hii kazi ni kazi yenye manufaa makubwa na itaweza kutusaidia sana kama nchi tuweze kusonga mbele na kusaidia kuitangaza nchi kwa kuwa na kiwanda kikubwa cha kuchanganya virutubishi,” alisema Waziri Mhagama.

Kwa upande wake Meneja Muandamizi wa Sanku, Gwao Omari Gwao amesema kampuni yao inasaidia wafanyabishara wadogo na wakati kufanya urutubishaji ambazo zimefunguliwa katika mikoa 26 Tanzania Bara na katika Halmashauri 142 Tanzania Bara.