Halmashauri zashindwa kukusanya kodi ya uzio

By Rose Jacob , Nipashe
Published at 11:26 AM May 01 2024
Mkuu wa TAKUKURU mkoani Mwanza, James Ruge
PICHA: MAKTABA
Mkuu wa TAKUKURU mkoani Mwanza, James Ruge

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Mwanza imesema halmashauri mkoani hapa zimeshindwa kukusanya kodi ya zuio kwa wananchi.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mkuu wa TAKUKURU mkoani hapa, James Ruge, amesema kuwa tatizo hilo linachangia kushuka kwa makusanyo ya mapato.

"TAKUKURU Mkoa wa Mwanza imefanya kazi ya uchambuzi wa mfumo wa kodi ya zuio na kufanikiwa kukusanya zaidi ya Shilingi milioni 68.164 katika halmashauri ya Ilemela kupitia Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA),"  amesema Ruge. 

Amesema taasisi hiyo pia imebaini mapungufu mbalimbali ikiwemo uelewa mdogo kwa wafanyabiashara wa kodi hiyo ya zuio na baadhi ya watoa huduma mitaani hususani mafundi ujenzi kutokuwa na namba ya mlipa kodi (TIN).