Mashujaa 6 wasioimbwa kwenye Ligi Kuu England

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 07:05 AM Apr 22 2024
Alexis Mac Allister.
Picha: Mtandaoni
Alexis Mac Allister.

MSIMU wa Ligi Kuu England, maarufu kama EPL, unapokaribia kumalizika, wachezaji wengi nyota wanatarajiwa kujitokeza katika michezo mikubwa zaidi ili kubaini taji litaishia wapi.

Kuanzia Kevin De Bruyne, Bukayo Saka hadi Mohamed Salah, timu sita za juu zina wachezaji wengi nyota ambao wanaweza kujitoa wakati huu, lakini zaidi ya klabu pia zinategemea mashujaa wengine kubeba mizigo pia.

Hapa tunawaangalia wachezaji sita mashujaa ambao hawaimbwi kwenye Ligi Kuu England twende sasa…

 Arsenal - Gabriel Magalhaes

Ingawa patina wake wa kati William Saliba anaweza kusifiwa zaidi, Gabriel ana msimu mzuri wa kimya kimya kwa Arsenal.

Akiwa ameshinda vita 72 vya anga na kuokoa hatari 77, bila shaka Mbrazil huyo ndiye beki hodari na anayeona hatari zaidi kwa kikosi cha Mikel Arteta.

Gabriel aliwasili Emirates mwaka 2020 akiwa na umri wa miaka 22, kutoka Lille ya Ufaransa. Amefunga mabao manne msimu huu akiwa na ‘Washikabunduki’ hao, na bao lake la hivi karibuni ni katika ushindi wa 6-0 dhidi ya West Ham, Februari.

 Liverpool - Alexis Mac Allister

Msimu huu umezingatia sana mchango wa wachezaji kama Mohamed Salah, Darwin Nunez na Virgil van Dijk katika harakati za Liverpool kuwania taji.

Lakini pia kelele nyingi zinapaswa kupigwa juu ya Alexis Mac Allister, akiwa amechangia kwa kiasi kikubwa katikati ya safu ya kati ya ‘Wekundu’ hao tangu ajiunge na klabu hiyo kwa ada ya pauni milioni 35.

Jurgen Klopp alifanya jukumu lake kumleta raia huyo wa Argentina pale Anfield msimu uliopita wa msjirs ys joto na amethibitisha thamani yake iwe ni katika kikosi cha kwanza au akitokea benchi. Katika mechi zake saba zilizopita za Ligi Kuu England, Mac Allister ameibuka na mabao matatu na asisti nne.

 Man City - Stefan Ortega

Ni vigumu kumtaja mtu yeyote katika timu ya Manchester City kama 'shujaa asiyejulikana,' lakini ikiwa kuna jina moja linalostahili kutambuliwa zaidi basi ni Stefan Ortega.

Ortega aliwasili Etihad majira ya joto yaliyopita huku Zack Steffen akiondoka kwa mkopo, na Mjerumani huyo amejidhihirisha kuwa msaidizi bora zaidi wa Ederson. Kwa hakika, baadhi ya mashabiki wa City bado wanahoji kwamba Ortega hutoa thamani zaidi kuliko Ederson kama kipa chaguo la kwanza.

Hakika aliwavutia mashabiki Jumamosi iliyopita, akimkwepa mshambuliaji wa Crystal Palace, Jean-Philippe Mateta na kuiwahi pasi kutoka kwa Rodri.

 Aston Villa - Matty Cash

Kuna utata labda ikizingatiwa kwamba yeye si jina la mara kwa mara katika kikosi cha kwanza na kwa sasa hana jeraha, lakini mchezaji huyo wa Kimataifa wa Poland, Matty Cash ni mlinzi anayetamaniwa na klabu kadhaa za Ligi Kuu England.

Mbio zake bila kuchoka na uchezaji wake wa kushambulia umekuwa muhimu kwa mafanikio ya Aston Villa msimu huu, huku vijana wa kocha Unai Emery wakiwania kufuzu kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao.

Cash alianza uchezaji wake katika Klabu ya Wycombe Wanderers na baadaye akademi ya FAB kabla ya kusaini mkataba wake wa kwanza wa soka la kulipwa pale Nottingham Forest, na kujiimarisha kama beki wa kulia wa kikosi cha kwanza. Alijiunga na Villa mnamo Septemba 2020.

 Tottenham Hotspur - Pedro Porro

Ni klabu gani ya Ligi Kuu England ambayo haiwezi kumtaka raia huyo wa Hispania kwenye timu yake?

Pedro Porro anastawi chini ya kocha Ange Postecoglou, akiwa amecheza mechi 27 akiwa na Tottenham Hotspur na kukamilisha dakika 90 kamili katika mechi 26.

Zaidi ya hayo, beki huyo wa kulia mwenye umri wa miaka 24, ametoa pasi za mabao saba, sawa na James Maddison na Brennan Johnson - dhihirisho la kweli la jinsi alivyo bora kwa Spurs msimu huu. 

Man United - Kobbie Mainoo

Katika msimu uliokumbwa na utendaji duni na kukatishwa tamaa kwa ‘Mashetani Wekundu’, Kobbie Mainoo ameibuka kuwa nyota.

Mainoo alianza mechi yake ya kwanza ya ligi kwa Manchester United msimu huu mwishoni mwa Novemba, katika ushindi wa 3-0 wa Ligi Kuu ugenini dhidi ya Everton, na kujishindia tuzo ya mchezaji bora wa mechi hiyo.

Hivi karibuni kinda huyo alimzidi akili kiungo wa kati, Enzo Fernandez wa Chelsea weye thamani ya pauni milioni 106 pale Stamford Bridge na pia alifunga bao zuri dhidi ya mahasimu wao Liverpool, na kuthibitisha kwa mara nyingine ni kwa nini wengi wamemtaka aanze katika safu ya kiungo ya Timu ya Taifa ya England, maarufu kama ‘Simba Watatu’ kwenye Euro 2024.