Kinana: tusiposhikamana kuna tatizo

By Maulid Mmbaga , Nipashe Jumapili
Published at 06:20 PM Apr 14 2024
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Bara Abdulrahman Kinana.
PICHA: MAULID MMBAGA
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Bara Abdulrahman Kinana.

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Bara Abdulrahman Kinana amesisitiza wanachama wa chama hicho kuwa na umoja katika utendaji akihadharisha kwamba wasiposhikamana kutakuwa na tatizo.

Ameyazungumza hayo leo mkoani Mara wakati wa kikao maalumu cha halmashauri ya CCM Serengeti, amesema miundo ikifanya kazi vizuri chama hicho kitaendelea kuwa na nguvu, kitaaminika na kukubalika.

Amesema chama hicho kinaendeshwa kwa utaratibu, kwa kufwata katiba, na pia kinakanuni kwa kila jambo ikiwemo uchaguzi, maadili na kanuni za utumishi, akisisitiza kuwa ndani ya CCM kila kitu kinaangaliwa na kinaandikwa.

"Ukiona mtu anafanya vitu visivyo hayo ni yake, pia tunaelekea kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu, ili tushinde vizuri viongozi lazima mtende haki usimpendelee mtu, musipandikize watu na musipokee rushwa kwani ni adui wa maendeleo," amesema Kinana.